Gari (RunX) kujizima ghafla

Gari (RunX) kujizima ghafla

MACHONDELA

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2018
Posts
940
Reaction score
1,573
Habari wakuu naomba msaada wenu,nakerwa sana

Gari yangu ni RunX huwa inatabia ya kujizima nikiwa barabaran,imenisababishia ajali mara moja na zingine nanusurika tu kwa maana gari hujizima nikiwa katika motion.

Nimejaribu kutafuta muafaka kwa sasa naelekea kukata tamaa, maana nimenunulishwa pump mpya bado tatizo lipo tu, mara naambiwa plug mara naambiwa umeme yaan shaghala baghala.

Naomba msaada wako au ushauri wa kitaalamu ili niepukane na keto hii maana kwa sasa Sina Raha kabisa na gari .
 
JITU LA MIRABA MINNE

Mi ningeanza na full diagnosis uzuri Runx ina OBD 2 port.

Ishawahi kuzima ikiwa silencer au inazima ikiwa kwenye mwendo?

Inazima mara ngapi kwa siku au kila baada ya mwendo gani au muda gani tokea uiwashe?

Labda ukifika speed flani ndio inazima, au ukiwa umeendesha sana ndio inazima?
 
Anza na diagnosis kama alivyosema mkuu hapo juu. Ikizima ukiweka switch on mshale wa temperature gauge unarudi kusoma kati au unakua umelala chini kabisa?
 
JITU LA MIRABA MINNE

Mi ningeanza na full diagnosis uzuri Runx ina OBD 2 port.

Ishawahi kuzima ikiwa silencer au inazima ikiwa kwenye mwendo?

Inazima mara ngapi kwa siku au kila baada ya mwendo gani au muda gani tokea uiwashe?

Labda ukifika speed flani ndio inazima, au ukiwa umeendesha sana ndio inazima?
Mara nyingi ikiwa kwenye mwendo na hasa slow motion eg kama kwenye folen
 
Mara nyingi ikiwa kwenye mwendo na hasa slow motion eg kama kwenye folen
Mimi sio fundi ila nilipatwa na tatizo kama hilo kwenye gari yangu.ilifikia kipindi nikiwa kwenye foleni naweka neutral afu napiga race ili isizime.
Tatizo ni silencer iko chini nenda kwa fundi anaipandisha yani gari ikiwa idle ile rotation inabidi isishuke zaidi ya 2.
 
nenda kaangalie mfumo wa hewa,
huenda una carbon au waswahili wanaita vumbi...kuna dawa yake maalumu ya kufasisha hiyo kitu ...na huenda usiione ukiingiza kwenye diagnos machine,
Hii ni kutokana na uzoefu wangu binafsi.
 
Back
Top Bottom