Gari ya diesel ikiwekwa petrol

Gari ya diesel ikiwekwa petrol

Kuna baadhi ya magari wahudumu hawajui kama hili ni la diesel na hili ni la petrol kwa mfano gari kama BMW 335d,
Mercedes-Benz E250 hivi zinatumia diesel kwa mwonekano kwa vile ni ndogo utajua inatumia petrol !!!
Kabisa wahudumu wengi wakiona gari ni dogo wamekariri ni ya petrol napata wateja wengi wa gari za aina hiyo kwa tatizo la kuwekewa petrol.asante kwa elimu zaidi
 
mbona mie napofika sheli hawaniulizagi kama nataka petrol au diesel? Naonaga wanaweka tu
 
Hii inatokea kwa magari mengi sana
Unakuta umeenda kituo cha mafuta Watoa huduma mara nyingi sana wanafanya makosa na kukuwekea petrol kwenye gar ya diesel au diesel kwenye gari ya petrol

Gari ya petrol kuwekwa diesel madhara yake yanajitokeza hapo hapo na pengine inaweza ata usiwake na gharama za kusafisha fuel system kwa gari ya petrol si kubwa sana zinabebeka.

Swala zito ni pale gari ya diesel ikiwekwa petrol
Gari itawaka na unaweza kutembea ata kilometer 8 had 10
Ila baada ya hapo utakuwa unaharibu system nzima ya mafuta kwa maana kuanzia pump na injector nozzles au injector units kwa magari makubwa

Nini kifanyike kama tu umegundua mapema umewekewa petrol kwenye gari ya diesel

1.usiwashe gari kabisa
2.shusha tank haraka na mwaga mafuta yotee na usafishe tank
3.weka diesel ya kutosha baada ya kusafisha tank
4.weka 500ml of injector cleaner solution
5.washa gari yako na iache ikae kwa muda idle
6.weka gia ondoka

Kama umeshindwa kujua na umeendesha gari yako ikiwa na petrol badala ya diesel baada ya muda mfupi gari itaanza kuleta miss na kutoa moshi mwingi mweusi na kupoteza nguvu yake ya awali

Nini kifanyike
1.peleka gari garage
2 .tank ishushwe na kusafishwa.
3.toa injector nozzle zote na pump
4.zipime injector na pump
Bila shaka zitakuwa zishakuwa damaged wasiliana nasi kwa maana tunamashine za kisasa za kupima nozzle na pumps za common rail na pia tunarepair pumps na injector nozzle za aina zote


Mawasiliano
0716505153
Dar es salaam-tabata magengeniView attachment 948832View attachment 948833View attachment 948834
upo sawa mkuu ila uja eleza kwa undani inakuaje gari ya diseli itembee kilomita 8 baadaa yakuekewa petrol . je nini kinisababisha gari ilo litembe ilihali ni special kwa matumizi ya disel……..
 
Moja ya suluhisho ni kuweka label kwenye mfuniko wa fuel tank. Gari nyingi sasa zinafanya hivyo toka kiwandani
 
Back
Top Bottom