Gari ya push to start kugoma kuwaka

Hiyo teknolojia inawezekana hata huko wazungu imewazingua ndo maana magari ya kuanzia 2015 wamerudisha ufunguo
 
leseni za kununua hiz
Kilicho ongelewa na chanzo cha tatizo havina uhusiano wowote na leseni , kwa sababu leseni haiendeshi gari mzee, kwa kilicho tokea hapo hata dereva mwenye class C1 na uzoefu wa miaka 100 barabarani kinaweza kumkuta , hilo ni swala la technology tu na technology sio ya baba yako mzee, waswahili tatizo ujuaji mwingi utadhani wanajua kumbe wapumbavu tu.
Wewe sio dereva.
Unawezaje kuendesha gari wakati huna sifa za udereva...gari inawashwa na boda boda wewe ndio uendeshe kazi ipo hapo
 
Dah yaan ukatoa buku tano duh...ndo kupata experience...next time issue kama hyo chukua funguo sogeza karibu kabisa na switch ya push to start Gari itawaka..shida signal zinakua zinaingiliana nA kufanya signal za funguo kuwa weak au kua interfered na kafanya system ya security ya ignition kushindwa kutambua code za funguo.
 
Ni kweli kabisa nami yalinikuta sehemu hiyohiyo na mgeni wangu tunaenda kukata ticket tazara ye anatalii tu Sasa kukaribia tazara hapohapo alaf kulikua na foleni kali tulikaa muda mrefu mpaka nikaamua nizime Gari.
Kimbembe foleni ilivyoanza kusogea kila nikiwasha Gari hola funguo haisensi nilipagawa na mahoni napigiwa mgeni wangu akakasirika akaniambia you need to service your car. Baada ya several attempts ndio likawaka.
Tukaingia ndani tazara pia kila nikibonyeza lock button kitu hairespond dash nikatoa funguo nikalock manually.
Nilipoteza credit kwa mbebe asee akaniona naendesha kimeo.
 
Hahahaha pole sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…