Gari ya Tundu Lissu ni kielelezo cha gharama za kuitoa CCM madarakani. CHADEMA tumnunulie Lissu gari jingine

Gari ya Tundu Lissu ni kielelezo cha gharama za kuitoa CCM madarakani. CHADEMA tumnunulie Lissu gari jingine

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Hili gari linatisha sana kuliangalia! Kinachonishangaza ni ujasiri wa Tundu Lissu kutaka kulitengeneza na kulitumia tena.

Gari hilo ni kielelezo cha jinsi ilivyo vigumu kuutoa madarakani mfumo CCM. Gari hilo lihifadhiwe makumbusho ya Taifa kwani ni alama ya ukombozi wa mtanzania.

Tundu Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa CDM anastahili kununuliwa gari mpya. Hapaswi kutengeneza ile gari ya zamani iliyo na matundu ya risasi.
 
Hakika nadhani ni Sahihi kwa Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA kuliweka MAKUMBUSHO Gari la Makamu Mwenyekito wake Mh.Tundu Lissu ktk MAKUMBUSHO ya CHAMA hicho .Kufanya hiyo kukiambatana na HISTORIA NZIMA ya namna alivyopigwa Risasi na WANAOJULIKANA yenye na Dereva wake itasaidia Vizazi vijavyo kuwajua Jinsi WATAWALA walivyokuwa Wanatumia RISASI kuua VIONGOZI wa UPINZANI.Historia hiyo itafanana na Historia ya Mapambano ya kutafuta Uhuru iliyofanywa na Mwl.Nyerere Miaka hiyo
Kwa wakati huu CHADEMA ipo kwenye Historia ya KUDAI KATIBA MPYA na TUME HURU ya UCHAGUZI.VIONGOZI wa CHADEMA lifanyie kazi WAZO hili ili vizazi vijavyo WAJUE mlikuwa MNAWINDWA na WATAWALA.
 
Makumbusho ipi. Hii ya Taifa? serikali itakubali!
 
Lakini hapa naomba nitofautiane na CHADEMA. Waliwahi kuoma Scotland yard na FBI waje kuifanyia uchunguzi ili wajue nani alitenda uhalifu ule.

Sasa Karuhusiwa kuichukua kwanini wasiwaite waje sasa kuichunguza ili kuwe na rechords kabla hawajafanya chochote na gari hiyo?
 
Back
Top Bottom