318horses
Member
- Jul 7, 2020
- 7
- 15
Habari za saa hizi wakuu, poleni na majukumu, gari yangu (corolla spacio) ilipata majanga iligongwa mbele vitu vyote vya mbele vikaharibika including fan, radiator na vyote vya mbele pale, so ikabidi iwe fitted with a new nosecut, baada ya hapo gari ikawa sawa, sasa kurudi barabarani gari inaenda nikifika tu kwenye foleni, geji ya temperature inaanza kupanda so inanibidi nipark nizime gari kwa muda kidogo then niendelee, badae nikaja kugundua feni ndo shida kwamba haifungui kwa wakati, lakini pia kuna kitu kikawa kinanitatiza kwasababu kuna muda ilikua inafungua, so ni kama ina mawenge kuna muda inafungua muda haifungui, nikampelekea fundi akasema ni switch ya feni akaweka nyingine, tatizo bado liko pale pale, kuongea na fundi tena anasema niende watoe thermostat gari iende bila thermostat, hapo sasa ndo nikawa na doubts, sasa sijajua nini shida nalileta kwenu wakuu tufunguane mawazo angalau, natanguliza shukrani
NB: sio kama feni haifungui kabisa, kuna muda inafungua kuna muda inafeli kufungua na hapo ndo overheat inapokuja
NB: sio kama feni haifungui kabisa, kuna muda inafungua kuna muda inafeli kufungua na hapo ndo overheat inapokuja