Mkuu
Steph JK , hebu tupe somo hapo.... umenigusa.
Gari yangu kwa sasa inavuma sana, yaani nafunga vioo full AC lakini mvumo unasikika, na ni kama upande wa kushoto nyuma.
Hapo awali niliwahi badilisha rubber ya driving shaft. Iliyokuwepo ilicrack na kuvuja, ndo fundi akaweka rubber nyingine na kujaza grease.
Hivi majuzi, taa ya ABS iliwaka kwa muda mfupi sana kama umbali wa kilomita 2 hivi. Asubuhi nilipowasha gari taa ya ABS haikuonekana tena, ikapotea hadi sasa.
Mvumo sio wa kawaida, upo juu hadi kero utadhani unaendesha lori. Nikahisi labda ni tairi, maana zilikuwa zimeisha. Nikaweka tairi mpya zote nne. Lakini bado gari inavuma mno. Kuanzia speed 60 tu au speed 80 kuendelea.
Lakini pia kule kwenye engine, ikishapata moto inatoa mlio wa kugonga hivi, yaani kama sauti ya kugonga hodi....'kohkohkohkoh'. Hako kamlio ni kwenye silencer/idle. Ikiwa kwenye mwendo hakasikiki.