Gari yangu ipo njiani inakuja, naombeni ushauri

Gari yangu ipo njiani inakuja, naombeni ushauri

Asante sana mkuu. Na kwa uzoefu wako, gari ya CFI usd 3500 mpaka niipate inaweza gharimu sh ngapi?
Kwa makadilio sahihi mkuu, naomba nipate make, model & mwaka wa kutengenezwa gari husika.
 
Nissan
xtrail - SUV
2008
CC 1990
1. ushuru za per tra calculator ni tsh. 8,102,364. Link: Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
2. Gharama za wakala wa meli (Local shipping line agency fee) haizidi $72 (Delivery Order fee, sumatra charges, car service charges) VAT included.
3. Wharfage charges, ambayo kwa sasa TRA wanaikusanya kwa niaba ya Bandari haizidi $60
4. TPA charges ni $125
5. Mwisho, ni gharama zetu za uwakala (agency fee), ambayo tunatoza tsh. 200,000.

Karibu sana mkuu, tunapatikana kwa anuani ifuatayo;

S.A Link Traders Ltd.
2nd Floor-Elite City building (Opposite Harbor View),
Samora Avenue/Morogoro Road,
Dar es Salaam- Tanzania.
Email: info@salink.co.tz
Mob: +255718 866 651 ( Call or Whatsapp ),
Our Website: www.salink.co.tz
Facebook page: S.A LINK Traders LTD
 
Wakuu,

Niliagiza gari, ndio namiliki gari kwa mara ya kwanza hivyo vitu vingi bado ni mshamba hivyo nahitaji ushauri wetu mniongoze.

Wakati naagiza gari nilishaangalia makadirio ya kodi kwenye website ya TRA, pesa yao ya kodi ipo tayari pia kuna milioni moja ya dharura. Sasa nahitaji kujua yafuatayo;

1. Gari ninayoagiza ni ya kibiashara, nataka iwe taxi. Je, kuna kodi za biashara ntatakiwa kulipa kabla au nitakuja kulipa nikianza biashara?

2. Gharama za ku clear gari bandarini pamoja na kulipa kampuni ya clearing zipoje?

3. Kampuni ipi ya clearing ni wazuri kwenye kutoa mizigo yako bandarini, wanafanya haraka na kwa uaminifu? huwa nasikia sana habari za kuchomolewa radio au vitu vingine kwenye gari

Naombeni mnitoe ushamba wakuu, mshamba wakati wa kwenda 🙂
Labda ungesema aina ya gari lenyewe (Aina, mwaka wa kuundwa, Ukubwa wa injini etc)

Ningeweza kusaidia kukupigia hesabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom