Gari za umeme pasua kichwa gharama za uendeshaji

Things do change...
Hata simu za mkononi zilipoingia zilikuwa aghali.....
Ngoja tumsubiri Mchina
 
Kuna prius ambayo.battery yake ni 2.5 mil
Prius kama una maana ya Toyota Prius ni hybrid, inatumia motor ya battery na engine ya petroli. Battery kwa motor ya umeme ni kubwa kuliko battery za kawaida na ni ghali ila siyo sawa na batteries za electric cars.
 
Hizi EV zikiingia bongo hawa mafundi wetu watazipiga sana shoti kmmk walai. Manake madungu jeshi yetu ya Europe walishayavuruga vya kutosha yako juu ya mawe yanasubiri spare, sasa haya ya umeme si ndio yatawaka moto kabisa kmmk.
 
Tesla ndio wanaonekana kuwa speed katika kuboresha teknolojia ya betrii na kwa makadilio mpaka 2030 watakuwa bafo hawawezi kukidhi mahitaji ya gari zao wenyewe, bado hawaja crack the secret to dry cathode coating so usitegemee gharama kushuka hivi karibuni.
 
Sisi huku Tanzania tunaosubiri used itakuaje? Haya magari ni mayai Tu sioni faida yake zaidi ya siasa Tu za wazungu za kukataa kutumia petroleum.
Kama ni mazingira kuna viwanda,mitambo ya kuchimba madini na vifaa vingine ambayo vinasababisha uharibifu wa mazingira

Magari ya kifala Sana haya sioni faida zake, gari haina mlio hata Ile vibe ya engine ikinguruma husikii Kwa kifupi haya magari ni baiskeli tu
 
Nimeona mwezi uliopita Tesla wamezindua pick up Yao ya Kwanza inaitwa cyber truck ina Sura mbaya kwelikweli
 
Kanunue gari za kichina za umeme bei nafuu.

Sio Kila gari ni la Kila mtu!

Wewe kama unaona Dolla 30,000 Kwa betri ni kubwa Kuna wengine hiyo ni bei ya konyagi tu!

Ukiona bidhaa kwako ni ghali jua wewe sio mteja mlengwa
 
Running cost ya EV ni ndogo kuliko ICE kwa muda mrefu.

Future ni Hybrid na EV.
 
Ndio maendeleo mkuu,
 
Sometimes hata hiyo miaka haifiki nishaona watu wanalalamika sana
 
Wapi huko wanauza battery ya prius kwa 2.5m mzee tukanunue maaana nmetoka kumfungia mteja wangu hata week haijapita kwa 4m tena hapo baada ya kupunguziwa toka 4.3m
Maisha yetu ya kibongo tunayajua wenyewe pamoja tunamiliki magari lkn sio muda wote utaweka full tank kuna kipindi huwa naweka ya BUKU 20-30 tena mara nyingi nafanya hivi..ingawa wadau wanasema kuwa magari ya umeme hayana gharama za uendeshaji bado nakataa ebu fikiria 4.3 milioni Kwaajili ya battery Tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…