Subiri betrii likifa ndio utajua tofauti ya wewe wa bongo na mbele ni ipi
Mkuu, labda nikuambie ...hizi hybrid kwenye battery pack yake inakua na modules kadhaa mfano yangu inakuja na module (cell 28) zenye volts 7.2 zilizo ungwa in series na kutengeneza total voltages 201.6 (this is minimum voltage...na kuna kua na computer inayo monitor voltage ya every individual block ya cell, sasa what happens ikitokea battery inashida utakuta ni cell specific ndo inashida so unafungua battery pack yako unaondoa hiyo cell mbovu unaweka nyingine maisha Yana songa....cell moja inauzwa kati 50,000 to 100,000 but buying individual cell unaeza ona ni cheap ila ukinunua kwa cell zote 28 at individual price inakua ni cost kubwa kuliko kununua the entire pack at tzs 1.5m... so options ni zako wewe...ukiwa DYI person kama mimi service ndogo mdogo kama nafanya mwenyewe maana ni kazi nyepesi sana..
Pia kama nivotangulia kusema awali maintenance ya hybrid car ni rahisi ni vitu vichache ndo vinaongezeka kama filter ya feni ya kupozea hybrid battery packs, lakini pia kusafisha carbon in case zikiwepo kwenye terminal... Lakini other than that hybrid car has less maintenance costs kuliko gari ya kawaida in terms of fuel consumption, oil change interval, 12 v battery lasting duration, brakes hubaduri kama gari ya kawaida (mie nimeendesha gari tangu ikiwa na km 50000 mpaka sasa ina 195,000+km bila kubadili pads za brake, engine haichoki kama gari ya kawaida, sina stress za gearbox na kuchange transmission fluid kama Gari ya kawaida, fen belt, sijui kufa kwa compressor ya ac, etc...
Ukitaka nunua gari hybrid kwa mtu ni kuwa makini unatakiwa uwe na fundi wa umeme apime kujua system faults gari maana kuna faults ukizikuta kidogo ni expensive ku repair mfano mfumo wa brake wa gari ya hybrid ni kama uliopo kwenye brevis na land cruiser v8 na nyingine zinakuja na electronic brake system kumbuka hybrid car si muda wote engine inafanya kazi hivo ili brake system yake ipate assistance ilibidi waweke mfumo wa kielectonic (brake by wire) ambayo inafanya kazi pamoja na regenerative brake mechanism so brake system ikifa hata mota tu unanunu system nzima ya ABS kwasababu inakuja kama unit moja so price ni 700k to 800k.
NB: nime attach screen ya data kuka kwenye application moja inaitwa dr prius ambayo huwa naiunganisha obd2 dangle kusoma data za battery yangu ie kama internal resistance ya batteries, voltages ya kila module, temperature ya battery pack, Delta State ot charge (Delta SOC) pamoja na State of charge ya battery yangu, then najua health ya 12v battery ukumbuke gari hii haitumii battery ya 12volts kuwasha engine kama gari ya kawaida hivo incase ikitokea battery. Hii ipo down si rahisi kujua kamq gari nyingine ambayo utaona starter inashindwa kuwasha gari but kwa hybrid car issue ni tofauti kidogo kwakua gari haina stator ya 12v inayowasha engine bali battery ya voti 12 hutumika ku switch on and off hybrid battery relays na ku power 12 volts system ya Gari yako kama taa, radio, wiper, etc hivo kwakua ni ngumu kujua health ya battery hyo ndogo maana wamekuwekea hiyo feature kwenye app ya dr prius ili iwe rahisi kujua what is going on... Pia application hii inakiruhusu kujua battery/cell gani ipo weak na ipi ipo strong hii kitu ni muhimu ndo maana app ina monitor voltage difference so ikitokea voltage difference ikafika 0.3 between cells basi gari itawasha taa ya warning,,, lakini pia app hii inakuwezesha kuona charging rate na discharging rate... Niishie hapa ila ni gari tamu na ina instant power because of electric motor
A