Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mwanzilishi wa shirika la kutoa misaada ya chakula la WCK, Jose Andres amesema kuuliwa kwa wafanyakazi wa shirika lake ilikuwa ni kitendo cha makusudi kilichofanywa na jeshi la Israel.
Katika mahojiano aliyofanya na redio moja ya Israel mwanzilishi huyo amesema magari matatu yalikuwa yakitoka kugawa misaada kwenye kambi ya Der El Balah jumla karibu tani 100 iliyoingia Gaza kwa njia ya bahari.
Ghafla gari hizo zilianza kushambuliwa kutoka angani japo zilikuw zikionesha nembo ya shirika hilo.Matokeo yake watoa misaada 7 waliokuwemo kwenye magari hayo wakauliwa. Waliouliwa ni kutoka mataifa ya Australia, Marekani, Canada, Poland na mfanyakazi mwenyeji wa kipalestina kutoka Rafah.
Kinyume na madai ya baadhi ya watu kuwa wapalestina wanaokufa kwa kupigwa kutoka angani huwa wamehifadhi wapiganaji wa Hamas, katika tukio hilo haioneshi kuwa kulikwa na Hamas aliyejificha kwenye magari hayo ya misaada.
Kuna habari kwamba kitendo cha mashirika ya kimataifa kugawa misaada kwa wenye njaa kimewaudhi viongozi wa Israel na katika siku za karibuni jeshi la Israel limekuwa likilalamika kuwa mashirika hayo yanagawa misaada bila kuwasilana nao kikamilifu.Hivyo kitendo cha kuyapiga magari hayo ni kama kitisho kwa mashirika hayo ili yaache kutoa misaada na ili wapalestina zaidi wafe kwa njaa.