Ngoja nijaribu kujibu kidogo kwa utaalamu wangu manaake mimi sijabase sana kwenye gesi zinazotengenezwa zaidi Niko kwenye field ya gesi asilia(zinazochimbwa) na madini
1: Ikipata ajali matanki yakapasuka basis hewa itaevaporate kuingia hewani tu na kujichanganya huko(hewani kuna CO2) ya kutosha tu kwahiyo itakua msaada kwa mimea imeongezewa hewa yao. CO2 haiwaki kwahiyo hakuna hatari ya kulipuka ikipinduka tanker. Tatizo labda kama ivuje gas ukiwa kwenye chumba ambacho hakiingizi wala kutoa hewa ndo utakufa lakini sio barabarani.
2: Hio hewa inaingizwa kwa pampu maalum baada ya kusindikwa(compressed) inabebwa na inaenda kushushwa kwenye matanki kwa ajili ya matumizi ya viwanda. Kituo nnachokijua ni TOL gases(Kampuni ya serikali hii zamani ikiitwa Tanzania Oxygen Limited wakati huo wanatengeneza Oxygen tu kwa ajili ya ma hospitali ila saivi imekua TOL Gases wanatengeneza ges nyingi zaidi kwa ajili ya kuchomelea,viwanda na za medical pia)
Wanatengeneza kiwandani kwao na gesi Nyingine kama Oxygen wanachimba kwenye visima vyao Tukuyu na wanauza mpaka Malawi Congo na Zimbabwe
3: Haiwezekani kupumulia kwenye mfuko na kuuza kwakua itakua ni kiwango kidogo sana. Ni mpaka ipitie process ya kugandamizwa kwa presha ili ifikie viwango.
4: Wataalamu wa kitanzania wapi na ndio wanafanya kazi hizo. Mmoja wako ni huyu anayeandika haya hapa
5: Kuna wataalamu wengine wamefungua kampuni zao ndio na wanatengeneza pia kwa mfano mbagala kuna Salina Oxygen Limited japokua bado hawawezi kushindana na TOL ndo ametawala soko