Kweli, hii di aidea nzuri sana na pia inamaslahi kwa hawa wakinamama na kwa nchi, ila si unajua mawazo ya viongozi wetu au hujui?
Watu wanajitahidi kuwa wabunifu lakini hakuna msaada wowote, nadhani ingekuwa poa kama serikali ingeangalia hili swala kwa kina na kufanya maamuzi yatakayotoa fursa za ajira.
Vipi kuhusu magari mengi yaliyopo hapa nchini yatafaa kutumia gongo(ethanol)? Ok, hii inawezekana kama kutakuwa na wataalam wa kubadilisha mfumo wa engine au sio?
Lakini je, vipi kuhusu upatikanaji wa hizi malighafi kwa ajili ya production ya hii gongo kuweza hudumia magari je zinatosha? Labda iwe inatengenezwa kwa kutumia miwa au hizo ndizi vipi hapa au ndo itakuwa aidea ya muda tu na baadae kushindikana kwa kukosekana kwa malighafi? Vipi haita leta usumbufu wa chakula kwa wale ndugu zetu wanaotumia ndizi kama chakula? Vipi kuhusu miwa, kama wazalishaji watakuwa wanauza sana kwa hawa watengenezaji wa hii ethanol kwa ajili matumizi ya magari kama nishati mbadala, si ndio tutakuwa na upungufu wa sukari? Ok nilisahau labda sio ishu sana kama tutokuwa hatunywi chai,, anyways tunaweza import ila daah hii si ndio ile inaitwa (inelastic good) sasa hapo vipi si ndio tatizo juu ya tatizo maana inelastic goods huhitajika hata kama ni bei gani,, nadhani hapa mshahara wa kabwela ndio utafika kikomo na kusababisha madeni juu ya madeni!