Hata ugunduliwe nini, kama akili zako bado zinakutuma kuwaa uwe na "leader" wakukufanyia mambo yako, basi utangoja sana. Kwanini wewe usiwe leader wa kujiongoza na kujiendeleza nafsi yako? tazama, hivi sasa, kuna wangapi ambao hali zao nzuri sana, na hali yenyewe kama mnavyosema ya nchi ya kamasikini, sasa fikiria ingekuwa nchi ya kitajiri hao walioweza kujienga kwenye umasikini wangekuwa wapi? nani anawaongoza?
Wacheni fikra mgando za kufikiria kushindwa kwako upate wa kumtupia lawama, hiyo ni namna ya kufikiri ya walioshindwa, kila akishindwa sababu ni fulani au fulani, hata siku moja hajitazami kwanini yeye mwenyewe kashindwa bila ya kumtegemea kiongozi? na wale walioweza wamewezaje na viongozi ndio haohao?