Rula ya Mafisadi
JF-Expert Member
- Dec 28, 2024
- 404
- 852
==
Binafsi Ninamuunga mkono Mhe TUNDU LISSU. na Nina sababu zangu za Msingi kutokana na Nini anakiwazia katika kuboresha mifumo ya Taasisi (Ndani ya CHADEMA). Leo nitajadili Kwa ufupi hoja yake ya kuondoa masharti ya ibara ya 6.3.2(c).
Hapo awali Kuondoa ukomo wa kuongoza Walikuwa sahihi Kwa wakati Ule Kwa sababu Chama kilikuwa Bado kichanga na hakikuwa na rasilimali Watu ya kutosha. Kwa sasa CHAMA kimepanuka mara dufu, sasa Kuna faida ya KUWEKA UKOMO WA KUONGOZA
1. Kwanza itamfanya kiongozi atimize majukumu yake Kwa Wakati na ufanisi (sababu Pana ukomo), na yeye kama kiongozi Mkuu wa chama ngazi husika (Msingi,Tawi,Kata,Jimbo,Wilaya, Mkoa,Kanda au Taifa) Akiwa na matarajio ya kujenga uimara na nguvu basi atatumia nguvu ya Ziada Ili kukimbizana na muda.
2. Pili, itapunguza ufuasi usio na msingi (UCHAWA Kwa Lugha isiyo rasmi) ambao hulenga kumpamba kiongozi Fulani. Hili limeanza kuonekana ndani ya Chama chetu. Kuna Haja ya kukomesha hili Kwa kubadili sehemu ya masharti ya katiba yetu
3. Itatuondolea uvivu wa kiutumishi Katika nafasi za uongozi ndani ya CHAMA. Kukiwa hakuna ukomo kiongozi anaweza bweteka na kuona Kwamba naweza ongoza Kwa awamu nyingi. Tukiweka ukomo Kila kiongozi Atakuwa anatazama muda uliobaki na hiyo Itakuwa kengeld muamsho tosha. Na ikumbukwe Kila kiongozi hupenda kuacha alama Kubwa kuwazidi Wengine kiuongozi
4. Itampa fursa kiongozi wa Wakati huo kufua na kuandaa vijana Wengi Ambao wanaweza tumika Kwa Siku za usoni baada ya muda wake kumalizika (sababu Pana ukomo)
5. Itaongeza Ari ya kuaminiana ndani ya taasisi. Kuondoa ukomo wa kuongoza Mara nyingi humfanya Kiongozi Kuwa Mfalme wa Taasisi. Na pengine hujenga makundi ambayo yatamlinda nyakati za chaguzi. Makundi haya hutumika vibaya na kupaka tope upande Ambao unashindana na mwenyekiti wa Wakati huo na kupelekea kutoaminiana ndani ya Chama. Hili kwetu limeanza kushamiri
Kwa vyovyote vile, kama tunaungana Katika kuboresha mifumo Yetu basi #TUNDU LISSU ni mgombea sahihi Kwa awamu hii.
Gaspar Sakalani