Invisible,
Lazima nikiri kuwa huyu Mwana muziki alinipita kushoto sana. Tatizo kubwa ni kuwa wakati akisitesa kwenye anga za Africa, mie nilikuwa nimeondoka kidogo na kuishi ughaibuni na huko kupata miziki ilikuwa kasheshe.
Ilitokea sherehe moja ya Watanzania na nikamuomba Marehemu Jafar wa JF.
MSIBA WA JAFAR WA JF (msiba wa siku nyingi) anitumie miziki kadhaa ya Kiafrica kwa sababu alikuwa amekwenda kusoma Belgium. Alinitumia kweli Cassete kadhaa na moja wapo ikiwa ni hiyo ya wimbo wa "ngoma ya kwetu." Kwenye sherehe nikampa DJ aupige na kwa shida sana akakubali. Ulipoanza tu kijana mmoja alikuja na kuanza kunieleza jinsi huo wimbo ulivyomrudisha mbali sana nyumbani. Kutoka hapo ndiyo nikawa nimeguswa na kuelewa sasa kumbe jamaa yupo juu sana.
Pana sehemu nilipata CD ya miziki ya Kiafrica na sikujali sana ndani kuna nini na akaja dada mmoja nikampa kopi. Mie ndani nilikuwa nimeupenda wimbo wa Dezo Dezo - Tshala Muana. Ila yeye ndani akaupenda wimbo wa Azalaki Awa. Akaniuliza kama ninazo nyingine na ukweli sikuwa nazo.
Kusema ukweli nimemfahamu huyu Mwana muziki juu juu tu na sikuwahi kuwa kwenye sherehe ambazo watu walicheza na kufurahia miziki yake. Kisa kingine cha kutokumpenda sana ni kule ku-Copy kwake sana Michael Jackson. Anyway, hilo ni tatizo langu mie ambaye nimeshazoea HIGH QUALITY ya Usanii kuanzia Recording, Video making, uchezaji, uvaaji nk.
Ila kwa hali ya nyumbani, nampa sifa sana kwani alijitahidi kuweka jina lake. Mara nyingi Wa-Congo wakipata visenti wanatumbua hadi vinaisha. Mwisho unaweza kumkuta kashakuwa Mbeba Box (sisemi anabeba box).
Kwa ufupi sina habari zake na labda nianze kufuatilia. Kwa Congo inaweza kuwa ngumu sana kwa Sababu Wacongo wanajali zaidi Mwanamuziki anayeimba kwa Kilingala au Kikongo tu. Ukianza kuimba lugha za watu, wanakuweka pembeni.
Nafikiri tatizo lake kubwa lilikuwa ni lilelile kama la Emeneya, Yondo Sister, Mayoni Mayaula, Defao nk kwa kutokuwa na Band yake maalumu na anabaki kuwa Mwanamuziki wa Kuunga-unga. Nafikiri hii huwa inaleta sana shida unapokwenda kwenye Concert LIVE na unakuwa huna wanamuziki waliopiga wimbo Original na mwisho hata uimbaji unakuwa mwingine kabisa utafikiri Band nyingine wanaku-copy. Watu wanakuchoka na kuanza kukimbia Concert zako na ndiyo mwisho wako kwa sababu kwa Africa huwezi kuishi kwa mauzo ya CD maana Wahindi ndiyo wanatajirika nazo, wewe utabaki na Concert na hizo sasa ukikosa, ndiyo umekwisha.
Sikonge, naamini nawe enzi hizi uliburudika nami; what happened to Gatho Beevans?