Gavana BOT aagiza benki zipunguze masharti ya mikopo na riba

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga amezitaka Benki na Taasisi za fedha kupunguza masharti ya mikopo na riba ili malengo yaliyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya kuwawezesha wananchi kiuchumi yaweze kutimia.

“Tumeelekeza benki ambazo hazishushi gharama za uendeshaji hazitaruhusiwa kutoa gawio mpaka zishuke hizo gharama ili tuone wananchi wanapata huduma bila kuwa na gharama zisizo eleweka,” - Profesa Luoga.
 
kwa kweli. tuna ajira ila masharti yake huwezi kukopa, na huku ndio tuko wengi.
 
Walione na deni la heslb,washushe %
 
BOT, fatilieni makato ya kibenk ni makubwa sana...

Yaani benki ifaidi 28,000 nzima kwenye kutoa 20mil

Hili hapana aiseee
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga amezitaka Benki na Taasisi za fedha kupunguza masharti ya mikopo na riba ili malengo yaliyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya kuwawezesha wananchi kiuchumi yaweze kutimia.

“Tumeelekeza benki ambazo hazishushi gharama za uendeshaji hazitaruhusiwa kutoa gawio mpaka zishuke hizo gharama ili tuone wananchi wanapata huduma bila kuwa na gharama zisizo eleweka,” - Profesa Luoga.
Mimi sijaelewa hapo kwenye hazitaruhusiwa kutoa gawio. Nahitaji ufafanuzi zaidi. Kwani zisipotoa gawio sii ndio vizuri kwa hizo benki?
 
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga amezitaka Benki na Taasisi za fedha kupunguza masharti ya mikopo na riba ili malengo yaliyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya kuwawezesha wananchi kiuchumi yaweze kutimia.

“Tumeelekeza benki ambazo hazishushi gharama za uendeshaji hazitaruhusiwa kutoa gawio mpaka zishuke hizo gharama ili tuone wananchi wanapata huduma bila kuwa na gharama zisizo eleweka,” - Profesa Luoga.
Hivi ukiwa na ideas ya miradi unakopesheka au ndio lazima mambo ya hati , nyumba , mashamba kwanza!!?
 
Hapo kwenye gawio mbona sijampata vizuri! Benki isipo toa gawio si ndio itafaidika zaidi? Au alikuwa anamaanisha haitapewa gawio?
 
Hivi ukiwa na ideas ya miradi unakopesheka au ndio lazima mambo ya hati , nyumba , mashamba kwanza!!?
Ata uwe na nyumba ya mamilion ya pesa kama huna kazi ya maana au biashara hawakukioeshi ng'oo.

Wengine tuna nyumba na mashamba ya urithhi lakini kwa kuwa ni mabodaboda wanasema hatukopesheki
 
Kwa riba chini ya 10% reducing balnc taasis nying za fedha zitashindwa kujiendesha
 
Gavana amemaanisha nini kuhusu kushusha garama za uendeshaji?

Mimi nadhani garama za uendeshaji hazihusiani na riba pamoja na garama za mkopo ambazo ndizo zinatukwaza wakopaji

Nadhani garama za uendeshaji ni kama, kulipa mishahara watumishi, kulipia majengo, umeme, maji na matumizi mengine ya ofisi ambayo hayahusiani na riba za mikopo
 
Umezungumza sahihi sana mkuu, gharama za uendeleshaji ni hizo kama ulivyochanganua. Lakini Gavana amezungumzia kuhusu punguzo la Riba maasharti ua kupata mikipo ili kuweza kuongeza idadi ya watu wanaochukua mikopo na hatimae kuweza ku boost uchumi.
 
Back
Top Bottom