Gavana wa Benki Kuu: Shughuli zote za Upatu ni haramu, tunawaonya wanaowaibia Wananchi

Gavana wa Benki Kuu: Shughuli zote za Upatu ni haramu, tunawaonya wanaowaibia Wananchi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Serikali imetoa onyo kuhusu shughuli za upatu, ambapo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Emmanuel Tutuba, amesema kwamba mtu yeyote anayeshiriki katika upatu kwa kukusanya fedha ili kuzigawa kwa wachache, huku akidai kuwa lengo ni kuvutia watu kuleta fedha zao bila kuwa na biashara halali ya kiuchumi, anakuwa amekiuka sheria za nchi.

Onyo hili amelitoa alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Machi 4, 2025.

Dkt. Tutuba amesisitiza kwamba upatu ni kinyume cha sheria na kwamba wananchi wanapaswa kuepuka kujihusisha na shughuli hizo zisizo rasmi za kifedha. “Mtu yeyote anayekusanya fedha kwa upatu anavunja sheria. Tunachukua hatua kwa kumkamata kila anayeendesha shughuli hizi haramu,” alionya.

Ameeleza kwamba shughuli yoyote ya kiuchumi halali inapaswa kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na utekelezaji wa majukumu yanayochangia maendeleo ya uchumi.

Aidha, Gavana huyo ameelekeza kwamba wananchi wanapaswa kutumia huduma za kifedha zilizothibitishwa na Benki Kuu, ikiwa ni pamoja na benki, taasisi ndogo za kifedha, na mitandao iliyoidhinishwa. Aliongeza kuwa ni muhimu kuwa na leseni kwa mtu yeyote anayekusudia kutoa huduma za kifedha.

Chanzo: TORCH MEDIA TZ
 
Back
Top Bottom