PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Benki kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza riba mpya kwa robo ya nne ya mwaka 2025 kupitia kamati ya sera ya fedha imesema kiwango cha Riba ya Benki Kuu (CBR) inasalia asilimia 5.75 katika robo ya nne ya mwaka inayoanza Oktoba hadi Desemba,2025.
Kiwango cha Riba cha Benki Kuu (CBR) huwa kinatumika na BoT katika shughuli zake na benki za biashara, ambazo zinapaswa kufuata sera hiyo ndani ya wigo uliowekwa na Benki Kuu.
Riba hiyo imetangazwa na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sera ya Fedha leo Oktoba 2,2025 katika makao makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika mkutano na viongozi wa benki na waandishi wa habari.
Soma zaidi: Gavana aipongeza CRDB Bank kwa kuthubutu kufanya mageuzi chanya ya kimataifa ktk huduma
Aidha amesema, uamuzi huu unatokana na mwenendo mzuri wa kuimarika kwa shughuli za kiuchumi na udhibiti wa mfumuko wa bei nchini, ambapo kamati hiyo ilikutana Oktoba 1,2025.
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilianza kutekeleza mfumo huu Januari,2024 badala ya mfumo uliokuwa unatumia ujazi wa fedha, Kupitia mfumo huu, Benki Kuu ya Tanzania huwa inatoa mwelekeo wa riba itakayotumika katika soko la fedha baina ya mabenki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki Tanzania (TBA), Theobald Sabi, ameipongeza Benki Kuu na Serikali kwa ujumla kwa kuendelea kusimamia vizuri uchumi wa nchi na ameishukuru BoT kwa ushirikiano mzuri kwa mabenki nchini ambao una mchango katika ustawi wa sekta ya fedha nchini.