Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Aliyekuwa Gavana wa nne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk Idris Rashid, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.
Dk Rashid aliyezaliwa mwaka 1948, wilayani Mbulu katika Mkoa wa Manyara, amefariki dunia usiku wa kuamkia Ijumaa ya Machi 13, 2026, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa za kifo chake, zimethibitishwa na mwanawe, Mohamed Idris, alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Ijumaa Machi 13, 2026.
“Ni kweli amefariki. Baba alikuwa anaugua saratani na amefariki katika Hospitali ya Shifaa, alikokuwa anapatiwa matibabu,” amesema.
Mohamed, amesema kiongozi huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), atazikwa kesho (Machi 14, 2026) mkoani Manyara.