Gawio la shs. kwa hisa CRDB

Gawio la shs. kwa hisa CRDB

Wakuuu mi sio mchumi kielimu ila kulingana na changamoto nimejukuta ninanunua na kuuza hisa mwanzo ilibipa changamoto sana yaani mwendo wa loss tu.. ila nikajifunza na saa naona ina maana, hisa inataka uwe mfuatiliaji, mvumilivu na kuwa muamuzi ila maamuzi yenye mashiko, nilikua nikiweka dolari 200 kama mtaji kwa hofu italiwa na kweli ilikua inaliwa kwa kuwa sikua najua..in short unaweza tengeneza hela 100% faida ama zaidi with days... utakuza mtaji ila pia kumbukeni kuna masharti ya kuwithdraw faida uliyoipata si kiwa unaweza with draw dola 1000 ulizotengeneza ndani ya wiki moja zote kwa mkupuo.. kwa sasa sijathubutu kabisa kuangalia hisa za hapa nyumbani za mbele kwa walio endelea safi kabusa
 
Leo nimepewa taarifa kuwa katika kikao cha Wanahisa kilichokaa mjini Arusha imeamuliwa kuwa gawio la kila hisa iwe shs. 10. Haingii akilini kwangu kutokana na faida ya Tshs.75bn iliyopatikana gawio inakuwa shs.10 kwa hisa moja. Ninatarajia kuuza hisa zangu zipatapazo 3500 ili nichukue ustaarabu mwingine. Ina maana katika hisa zangu 3500 gawio langu ni shs.35,000 bado kodi. Kwangu naona kama tusi. Hata akaunti yangu nitahamisha kutoka CRDB.

Hizo hisa zako 3,500 zina thamani gani? Acha makelele wewe kawekeze kwenye biashara ya vitumbua na vijisenti vyako.
 
Inamaana shiling 140 wame reinvest.. Kwa hiyo dhamani ya kila hisa yako moja inapaswa kupanda kwa shiling 140.. Uwekezaji wa hisa ni for long term ila kama unawekeza kutegemea kuvuna kwa hisa 3500 bora tu ukaweke fixed utapata hiyo asilimia yako. Hisa ni kwamba siku utaomua kuuza ndo unapaswa kupata faida kama bei uliyonunulia ilikuwa ndogo. Kwa hiyo unaweza kujikuta ukiuza hela unayopata ikawa zaidi ya fixed deposit..
 
Leo nimepewa taarifa kuwa katika kikao cha Wanahisa kilichokaa mjini Arusha imeamuliwa kuwa gawio la kila hisa iwe shs. 10. Haingii akilini kwangu kutokana na faida ya Tshs.75bn iliyopatikana gawio inakuwa shs.10 kwa hisa moja. Ninatarajia kuuza hisa zangu zipatapazo 3500 ili nichukue ustaarabu mwingine. Ina maana katika hisa zangu 3500 gawio langu ni shs.35,000 bado kodi. Kwangu naona kama tusi. Hata akaunti yangu nitahamisha kutoka CRDB.
..hakuna bank nayoichukia kama CRDB
 
Tangu serikali watoe pesa kwenye commercial bank CRDB wana tatizo la liquidity sana
 
Ehmmm sasa apa majanga, kama ndo haya mambo. Je wale wenzangu wa vodacom shares mna information yoyotee...?
 
Mkuu uwekezaji mzuri ni kununua viwanja vilivyopimwa, kwa sababu ardhi inaongezeka thamani kila siku, mimi nilikuwa na viwanja vinne hapa dar ambavyo nilivinunua miaka miwili iliyopita kwa milioni nane nimeviuza majuzi kwa milioni 40
Tz haieleweki. Ardhi ni mali ya raisi
 
Ungeuza leo mkuu ungepata laki saba tu. 3500 × 200 =700,000

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Aliyekwambia hisa ni asset nani? huna elimu juu ya umiliki wa hisa, huwezi kununua hisa ili kupata gawio, hisa ni kama bidhaa unaangalia asubuhi wapi inapatikana kwa bei ya chini, unanunua mchana ikipanda unauza unahesabu balance iliyobaki, unatafuta bar yenye warembo wazuri unatulia kusubiri siku nyingine. Hiyo ndi biashara ya hisa.
Hahahhaahahahahah. Unatafuta Bar wenye Warembo wazuri[emoji23]

Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
 
Uwekezaji kwenye hisa sio sawa na servings account, ambapo una huhakika WA kupata faida. Uwekezaji kwenye hisa hauna guarantee, tena unabahati Umepata hiyo sh.10/share.
 
Crdb wanachezea pesa za watu, Mimi nilinunua za 2m nikauza zote coz zinashuka tu thamani

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kazi ya hisa sio kusubiri dividends ni kuuza na kununua hapo ndo utaona faida yake hiyo dividends ni watu wenye mtaji mkubwa. Halafu kampuni sio lazima zitoe Gawio sasa kama unanunua hisa ili upewe Gawio ni kujitafutia stress

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Wakuuu mi sio mchumi kielimu ila kulingana na changamoto nimejukuta ninanunua na kuuza hisa mwanzo ilibipa changamoto sana yaani mwendo wa loss tu.. ila nikajifunza na saa naona ina maana, hisa inataka uwe mfuatiliaji, mvumilivu na kuwa muamuzi ila maamuzi yenye mashiko, nilikua nikiweka dolari 200 kama mtaji kwa hofu italiwa na kweli ilikua inaliwa kwa kuwa sikua najua..in short unaweza tengeneza hela 100% faida ama zaidi with days... utakuza mtaji ila pia kumbukeni kuna masharti ya kuwithdraw faida uliyoipata si kiwa unaweza with draw dola 1000 ulizotengeneza ndani ya wiki moja zote kwa mkupuo.. kwa sasa sijathubutu kabisa kuangalia hisa za hapa nyumbani za mbele kwa walio endelea safi kabusa
Hii nzuri lakini inahitaji elimu zaidi
Yaani biashara ya hisa uwe na milioni kadhaa ndo utafaidika
 
Back
Top Bottom