Gawio la Tshs. 11.93 kwa hisa linasikitisha, Vodacom inafanya biashara kubwa kuzidi baadhi ya mabenki

Mimi ni Mwanahisa wa Vodacom na nimepata taarifa kuwa mkutano mkuu wa Wanahisa wa Vodacom utafanyika tarehe 11 Septemba, 2024 kielekroniki. Binafsi nina hakika Vodacom inafanya biashara kubwa hata kuzidi baadhi ya Mabenki lakini kinachosikitisha ni gawio walilotangaza ya Tshs. 11.93 kwa kila hisa.

Kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na biashara yao. Mfano kama NMB wanatoa zaidi ya T.shs. 100 kwa kila hisa kwa nini wao watoe kiasi hicho ambacho ni kidogo sana. Ninawaomba njia ya kuchukua ili nitoke kuwa mwanahisa wa Vodacom na nipeleke hisa zangu NMB.

Inasikitisha sana.
Mkuu ni kweli. Hawajawahi toa gawio la kuridhisha.
Nimejaribu kuuza hisa zangu hata kwa bei ya hasara lakini hakuna wateja!
 
Mimi ni Mwanahisa wa Vodacom na nimepata taarifa kuwa mkutano mkuu wa Wanahisa wa Vodacom utafanyika tarehe 11 Septemba, 2024 kielekroniki. Binafsi nina hakika Vodacom inafanya biashara kubwa hata kuzidi baadhi ya Mabenki lakini kinachosikitisha ni gawio walilotangaza ya Tshs. 11.93 kwa kila hisa.

Kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na biashara yao. Mfano kama NMB wanatoa zaidi ya T.shs. 100 kwa kila hisa kwa nini wao watoe kiasi hicho ambacho ni kidogo sana. Ninawaomba njia ya kuchukua ili nitoke kuwa mwanahisa wa Vodacom na nipeleke hisa zangu NMB.

Inasikitisha sana.
Wenye pesa za mboga watajitoa wenyewe
 
Kwahio ukiwa na hisa 10,000 unalamba 110,000 ndugu muwekezaji
 
Una maana gani? Wakati CRDB hisa watu wananunua kwa Tsh 500 kwa kila hisa na gawio lao mwaka huu ni Tsh 50 kwa kils hisa. Vodacom watu walinunua kwa Tsh 850 kwa hisa mwaka 2017 lakini gawio lao kila mwaka halifiki Tsh 20.
Michezo michafu ya TRA na washirika wake.
 
Una maana gani? Wakati CRDB hisa watu wananunua kwa Tsh 500 kwa kila hisa na gawio lao mwaka huu ni Tsh 50 kwa kils hisa. Vodacom watu walinunua kwa Tsh 850 kwa hisa mwaka 2017 lakini gawio lao kila mwaka halifiki Tsh 20.
Mahesabu ya watu haya ? Shilingi 50 ????
 
Siku nikiishiwa na nguvu hata za kutoka nje ndo nitaweka Tsh 500 yangu sehemu nikisubiria Tsh 50 gawio kwa mwaka. Kwa sasa nikiwa niko timamu kiafya na kiakili nitapambana na biashara zangu hizihizi.
 
Back
Top Bottom