Gazeti la An-nuur lamuadhimisha Kleist Abdulwahid Sykes (1950 - 2017)

Ralph...
Popote panapo dhulma malalamiko yatakuwepo.
Huenda wewe huyaoni wala kuyahisi lakini hii haina maana kuwa hakuna malalamiko.
Sheikh nimekuelewa. Labda nataka kuelewa pia ambacho hujakisema wazi, kuwa watu wanalalamika lakini siyo kwa mtindo ule niliozowea kusikia. Lakini kwa hali ya sasa, nilitarajia malalamiko zaidi kwa msisitizo na jitihada kubwa kuliko wakati mwingine wowote, maana huyu wa sasa anauma bila kupuliza!
 
Malaleo,
Sijakimbilia popote huo ndiyo mtihani tuliokuwa tukifanya.
Kiswahili unanisoma hapa.
Nich name yangu sijaandika Malaleo ni Mlaleo Kiswahili kwako ni Shida bora uandike kwa lugha Yako ya Kimanyema ila Nahisi utakuwa wewe ni Muha wa Burundi kwa uandishi huo wa Malaleo?

Naku advice kajifunze upya Kiswahili kwa uandishi wako huu!
 
Ralph...
Ahasante sana kaka.
Unaitwa Sheikh unaitikia tu kwa furaha wewe ni Sheikh? wa Wapi? au wa Msikiti wa Manyema maana nasikia hapewi mtu uongozi kama si Mmanyema mule
 
Unaitwa Sheikh unaitikia tu kwa furaha wewe ni Sheikh? wa Wapi? au wa Msikiti wa Manyema maana nasikia hapewi mtu uongozi kama si Mmanyema mule
Mlaleo,
Nakutaka radhi kwa kukosea kuandika jina lako.

Mimi si sheikh hata kidogo na nimepata kueleza hapa kuwa sijasoma
kwa kiwango cha kuitwa sheikh.

Mimi kama nitaitikia kwa jina la sheikh naitika kwa ajili yz uzee wangu.

Kweli Msikiti wa Manyema tunapendelea sana uongozi uwe kwetu ingawa
kuna watu ni viongozi wa msikiti lakini si Wamanyema.

Imam wa Msikti wa Manyema anachaguliwa na kunakuwa na maimamu
kadhaaa.


Sheikh Hussein Juma

Katika Dar es Salaam ya 1940s hadi kufikia 1980s katika masheikh wakubwa
wa Dar es Salaam alikuwa Sheikh Hussein Juma baba yake Yahya Hussein.

Basi yeye alikuwa wala haswali Msikti wa Manyema wala alikuwa haombi uimamu.

Lakini wakichagua maimamu kabla ya uchaguzi kwanza linawekwa jina la
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Manyema, Sheikh Hussein Juma na wala haipigwi kura.

Jina linawekwa juu kisha ndipo wanajadili waombaji.

Jina la Hussein Juma linakuwa Imam No. 1 Msikiti wa Manyema kisha ndipo yanafuata
majina na masheikh wengine.

Sheikh Hussein Juma alikuwa anazaa watoto ''superbright,'' kama Prof. Mansour
(Mathematics) na Muhidin aliyesoma Makerere ambae alikuwa Inspector wa Police wakati
waukoloni na alikuwa na mabinti wazuri wa sifa kama marehemu Salama, Husna, Nuru na
wengine wengi.

Katika watoto wa sheikh mmoja alikuwa rafiki yangu brilliant footballer marehemu Salum
Hussein
jina la mpira tukimuita Livingstone Madegwa.

Huyu Madegwa alikuwa mchezaji wa timu ya Gossage ya Kenya.

Nakumbuka mmoja wa maimamu vijana wa Msikiti wa Manyema alikuwa rafiki yangu
marehemu Hamisi Tumbo na yeye aliomba uimamu wakusalisha Salat Fajr.
 
[QUOTE="Mlaleo, post: 24754930, member: 56852"]Nich name yangu sijaandika Malaleo ni Mlaleo Kiswahili kwako ni Shida bora uandike kwa lugha Yako ya Kimanyema ila Nahisi utakuwa wewe ni Muha wa Burundi kwa uandishi huo wa Malaleo?

Naku advice kajifunze upya Kiswahili kwa uandishi wako huu![/QUOTE]
Mlaleo,
Nimepokea ushauri wako nitajifunza lugha ya Kiswahili.

Sidhani kama kuna tatizo la mie kuwa Muha kwani hao wote hawakuomba
wawe kabila gani ni Allah mwenyewe ndiyo kawapangia na akasema kuwa
katutofautisha katika makabila ili tujuane na mbora ni yule amchae Allah.

Kuna haja ya mie kukueleza kuhusu huo wino mwekundu?
Unajua tofauti ya ''advice'' na ''advise?''
 
Chief....awamu hii kila mtu anahangaika na maisha ule ujinga wa watu wanakaa miguu juu wakishashiba na kufanya discussions za kijinga hakuna,watu maisha yamewafundisha ninini maana ya ya utaifa,kile kipindi cha watu wanabangaiza mpaka saa9 alaa'sir mfuko umeshanona na kwenda kwenye vibaraza kujazana ujinga hakipo sasa hivi ni kuhangaika mtu akitoka huko ni nyumbani kwa mkewe chai iko wapi chakula kuoga anakitafuta kitanda anaingoja kesho kama atajaaliwa kwenda kuhangaika tena.bro shibe inampa mtu kiburi hayo yote ya ubaguzi wa kidini sijui nini hayajawahi kuwepo hapa kwetu kilichokuwa kinatokea ni kwasababu maisha yalikuwa rahisi ndo maana watu walipata muda wa kuzungumza ujinga huo ila hatimaye tumeanza kujua na kuelewa kwamba uwepo wa rais au waziri mwenye imani sawa na mimi haunisaidii chochote linapokuja suala la maisha na hali hii acha iendelee ili kizazi kijacho kisije kikarithi ujinga ule.
 

Sir...
Ninapomsoma mtu huwa najenga katika fikra yangu huyu mtu atakuwaje.
Wapi anatoka, nini inaweza kuwa msimamo wake katika matatizo yaliyopo.

Kwa nini anasema haya anayosema.

Napita kwingi na hii inanisaidia kuweza kumjua mtu fikra yake na mengi
mengine.

Nikifika hapa nakuwa na picha kamili na hata kufahamu uwezo wake katika
kufikiri.

Lugha yako na maneno, ''ujinga,'' na uandishi wa mfano wako umenisaidia sana.

Ikiwa naona anastahili kujibiwa basi nitajibu la ikiwa nahisi haifai kumjibu hivyo
ndivyo inavyokuwa.

Waswahili tuna msemo: ''Mdomo haumkatai bwana wake.''
 
.....ila mwisho wa siku kila mtu ameelewa yanayompasa ktk u-Tanzania wake na umoja wetu,mimi nasema hali hii iendelee ili kila mtu awe busy na shughuli zake tukikutana kama ni kijadiliana iwe ni masuala ya msingi yanayohusu maisha yetu siyo kuzungumza nani kachaguliwa nani hajachaguliwa na sababu nyiiingi za uwongo na kweli.
 
Mkuu Mohamed Said umeulizwa mtoto wa miaka 11 alipigania vipi uhuru?
 
Mkuu Mohamed Said umeulizwa mtoto wa miaka 11 alipigania vipi uhuru?
Lusungo,
Hilo swali nitaulizwaje ilhali sijapatapo kusema kuwa Kleist mjukuu alipigania uhuru?

Ingefaa wewe ukamuuliza muulizaji wapi imesemwa Kleist Abdulwahid alipigania
uhuru?

Sasa ikisadifu mie ndiyo niliyosema dhahiri itakuwa nimekosea vinginevyo kama sijasema
hiyo itakuwa yeye msomaji hakuelewa na hili ni jambo la kawaida.
 
Sir...
Nilisema kuwa kabla sijamjibu mtu nampima kutaka kujua yukoje.
Ila nitakueleza kitu.

Huwezi kupuuza mgawanyo wa madaraka katika nchi.

Laiti ikiwa utaelemea upande mmoja lazima wale wanaopinjika bila
shaka watauliza.
 
Napenda sana hoja zako za nguvu na sio nguvu za hoja. Ila unaniangusha pale unapoamua kujibu kila comment hata za wale wanaoonekana ni mentor hadi wanatuchosha kuzipata fact.
 
Nich name yangu sijaandika Malaleo ni Mlaleo Kiswahili kwako ni Shida bora uandike kwa lugha Yako ya Kimanyema ila Nahisi utakuwa wewe ni Muha wa Burundi kwa uandishi huo wa Malaleo?

Naku advice kajifunze upya Kiswahili kwa uandishi wako huu!
mzee hujajibu swali,unajua tofauti kati ya. " advice" na " advise"
 
naona unampa elimu ya historia na sarufi kwa mpigo hahaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…