Gazeti la MwanaHALISI lafungiwa kwa miaka miwili, wahukumiwa kwa kuandika habari za uzushi kuhusu Mwakyembe na Makinikia

Naona hiii nchi ifanywe tu ya chama kimoja, kama kusema na kukosoa serikali ni dhambi kwa kweli tunaelekea kubaya, wacha watumie jeshi, polisi, uwingi wao bungeni, na vyombo vyote vya kukandamiza uhuru wa habari lakini kuna mwisho na kuna Mungu anayehukumu kwa haki.
 
Miaka miwili ?Uhuru wa vyombo vya habari upo Wapi ?Tanzania kama Uturuki.


Uhuru lazima uendane na haki .

Ecoutes moi, Ma Cheri Victoire, l'indépendance tourjour s'arccorder avec le droit.

Uhuru wamepewe ila wao wasijiandikie tu habari za kufikirika.
 
safi sana tumechoka kusoma uongo.warudi tena shule hao waandishi wa hilo gazeti

Uongo uko wapi hapo? Hasira za Maelezo zinatokana tu na makala (ambayo wao Maelezo wameiita kuwa habari) ambayo ni maoni ya mwandishi aliyetumia hoja za Lissu alipokuwa akijitetea mtandaoni baada ya maCCM kuanza kumshambulia yakidai kuwa sio mzalendo. Katika maelezo yake yale Lissu anaeleza jinsi alivyo mzalendo kuliko Rais. Hapo ndipo kuna hasira za Maelezo.

Huu ni uoga na ni unafiki wa kupindukia. Dk Abbas sasa anajikomba to the maximum kwa mkuu wa nchi. Ile makala ya Ngurumo ni ukosoaji wa kawaida kabisa. Inawezekana kweli mmechoka kwa namna mnavyozidiwa hoja, lakini kuchoka kwenu ndiko kunasababishwa nyie mzidi kuchokwa!
 
Hii kesi kweli.mwanahalisi.wataishinda?? Maan mtetezi wetu bado yuko kenya anaumwa. Mungu mponye haraka Tundu Lissu wetu
 
Kumbe kweli makinikia yamekwama maana si kwa hizi hasira, mnaju mtu aliyeshindwa jambo anavyokuwa na kisirani utadhani wewe ndio umeshababisha ashindwe.
 
Tumezoea sarakasi za awamu hii........... Ukisema ukweli hehehehe . Tuko bussy kumchangia kaka wa taifa tundu lissu tushafikisha dola 20 elf zinafaa kufika 50$ hima watz mchangieni
 
Mkuu hakuna uhuru usio na mipaka! Hivyo hawawezi wakaandika habari hata ya uongo eti kwa sababu ya uhuru wa vyombo vya habari. Lazima waandike habari ya kweli si ya kutunga!
 
pamoja na kuonywa kote huko,lakini kubenea kaendelea kuwa kichwa ngumu ..hakika upandacho ndicho uvunacho..
benchi la miaka miwili ni kuuwana kiwango aisee...
 
mdada wahuni hao, hawajakupata ukaingia kona zao, ni blackmailer, wazushi

hivi wanaweza wakasema wewe ni mwanaume!! na wakaweka evidence zao

kuweni wakweli tu, acha ushabiki
Lakini mara zote mahakama imekuwa ikithibitisha kuwa sio wazushi. Na mlivyo watu wa ajabu hata Mawio walipoandika kuhusu aliyekuwa naibu waziri Ngonyani Mawio lilifungiwa mkashangilia, lakini jambo la ajabu hata juzi waziri huyo huyo alipotakiwa na Magufuli ajiuzulu baada ya kutajwa na Kamati ya Bunge kwenye madini kwa jambo lile lile lililoandikwa na Mawio likafungiwa, mkashangilia tena. Nchi hii inaangamia kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wa aina yenu!
 
Kwa kulifungia Mwanahalisi,Sauti za wananchi hazitapaa hewani? Hapa kazi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…