Gazeti la MwanaHALISI lafungiwa kwa miaka miwili, wahukumiwa kwa kuandika habari za uzushi kuhusu Mwakyembe na Makinikia

Kuna fani huwa haikosei?
Wahandisi wanaporomosha majumba, wanajeshi yanatokea ya mbagala na gongolamboto, madereva ndio kila siku, madaktari wengine hupasua kichwa badala ya mguu, mahakamani rufaa nyingi tu zinashinda ikimaanisha walihukumiwa kimakosa, mashuleni ndio usiseme! Kwa mfano "siasa ni kilimo"

Kwenye siasa, kwa mambo ccm inayoyafanya hayajawahi kuleta faida kwa nchi! Si mkukuta wala mkurabita.
Ugatuaji wa madaraka mikoani umemalizwa na pushup za jukwaani.

Boriti jichoni mwa nchi hii ni CCM, tusihangaike na vibanzi machoni mwa tasnia nchini.
 
Fungia kabisa hata miaka mitano
 
Miaka miwili ?Uhuru wa vyombo vya habari upo Wapi ?Tanzania kama Uturuki.
Acha uongo haya mambo yako nchi zote, tena Marekani Trump huwa anafukuza kabisa wandishi wa gazeti la The New York Times kwenye press zake
 

Safi sana na uamuzi huu umechelewa sana.
 
Subiria huo mwisho mpaka unazeeka
Mwisho upo, kama usingekuwepo Bashite Maliyamungu asingehaha kutoa Rushwa kuzuia walitaka kusoma Albadri, wanajua Albadri ingesomwa vizuri bila vikwazo yy Lipumba na kikundi chao wakiwemo kubwa jinga Le mutuz wasingepona.
 
Kama wanaadika uongo wawapeleke mahakamani
Hata wao wanaweza kwenda mahakamani kama wameonewa. Hata hivyo kuna mambo mengine yanaisha hata bila kupelekwa mahakamani na mengine kutolewa mahakamani kwa ajili ya kupatana nje ya mahakama au kuadhibiwa kwa namna hiyo hiyo.
 
Poti lini utakuja nyumbani! December nakuja. Nasikia hali mbaya sana

Poti nimetoka mara ya mwisho ' Uzanakini ' mwaka 2009 na mpaka sasa bado sijaenda na najua kabisa kwamba ' mizimu ' yetu ile mikali ya ' Kizanaki ' itakuwa imekasirika mno na Mimi. Hata hivyo namalizia ' michakato ' fulani ili angala ndani ya miaka mitatu au mitano ijayo niweze kwenda ' nikatambike ' kwani naona kama vile ' Betri ' zangu zimeisha ' chaji ' Poti.

Ukienda nisalimie sana Wazanaki wenzangu wote wa kuanzia Butuguri, Buhemba na Butiama waambie Kijana wao GENTAMYCINE a.k.a The Brain of Zanaki nipo, nawakumbuka na ninawawakilisha vizuri sana katika mambo mbalimbali kama vile ambavyo ' naturally ' Wazanaki ni Watu very intelligent, humble, committed, brave, daring, visionary, hardworking, philosopher Kings and fearless.

Mkuu leo umenifanya niwakumbuke sana Ndugu zangu ' Wazanaki ' na Mkoa wangu mzuri wa Mara ( Musoma )

Najua kwa ' bandiko ' hili ' Washamba ' wa kutoka Kagera, Kigoma, Singida na Dodoma kwa Warangi ' watanuna ' ile mbaya kwani walitamani mno GENTAMYCINE nitokee katika hiyo Mikoa yao ili na wao basi angalau ' waringe ' na Mtu ambaye kiukweli ni ' Purely Talented and Charismatic Fella '.

Kila la kheri Poti wangu.
 
Miaka miwili ?Uhuru wa vyombo vya habari upo Wapi ?Tanzania kama Uturuki.
Uhuru ni HAKI ya kila mmoja wetu, na kila haki ina WAJIBU. Wajibu wako ndio haki ya mwingine. Hatuna haki ya kuandikiwa habari za uongo na uzushi. Waandishi wanatupokonya haki zetu kwa kusingizia uhuru wao. Kama habari zao za kweli kwa nini waombe radhi?
 
Fungieni magazeti yote tusome Uhuru na mzalendo na habari leo tu! Ila tupatiwe:
-Milioni hamsini zetu kila kijiji
-Computer kwenye shule zetu zote za msingi na sekondari
-Noah kila mtanzania kwa sababu tumeshinda mjadala wa makinikia
-Viwanda kila kata

Au kama hakuna vyote hivyo uhuru waandike mungu magufuli rais bora duniani basi araa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…