Gazeti la Mwananchi, Ni lini Mbowe alitangaza kugombea Urais wa Tanzania 2025?

Ulisoma kabla ya kupost? Mana haieleweki umeandika nn haswa
 
Lissu katamka hadharani, na Mbowe katamkia wapi?
Lisu ni mropokaji, mwenye viherehere, siasa za chuki na uchochezi, hana staha, mpenda vurugu, asiye na adabu kwa binadamu wenzake, anaamini yeye ndiye atakuwa rais wa JMT 2025 iwe jua iwe mvua etc

Mbowe yuko tofauti. Hana vihere here. Siasa zake ni staha na ni gwiji wa kutunga hoja zenye mashiko na ushawishi kwa mtu ye yote bila kuudhi au kutweza mtu. Kipindi cha kutoa nia ya kuwania kugombea uraisi a
kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 bado haujafika. Hivyo hawezi kukurupuka kusema hivyo kwa sasa.

Ukweli ni kwamba TL anawachafulia chama chenu kwa kukifanya kionekane kama chama cha wahuni, chama cha kuvuruga nchi badala ya kujenga nchi. Mguu wake mmoja uko Tanzania na ule wa pili uko Ubelgiji na Marekani. Akikinukisha hapa Tanzania huwa hachelewi kukimbilia Ubelgiji au Marekani. Pakitulia hurudi tena kuja kukinukisha.

TL anajua kabisa kwamba akigombea ubunge huko kwao Singida hawezi kupita, ataambulia aibu ya kushindwa vibaya. Hivyo kiti pekee anacho tamani agombee ni hicho cha uraisi ambacho anajua atashindwa vibaya lakini hataaibika kwani atasingizia kura zake zimeibiwa kwa mtindo wa Nape style!
 
Kutangaza nia ya kugombea Urais tena kwa kufuata utaratibu wa Chama chake ni Uropokaji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…