Gazeti la Mwananchi online lafungiwa miezi sita na kulipishwa faini milioni 5 kwa kupotosha

Gazeti la Mwananchi online lafungiwa miezi sita na kulipishwa faini milioni 5 kwa kupotosha

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania kuiptia Kamati ya Maudhui imesitisha leseni ya utoaji wa huduma za maudhui mtandaoni ya Mwananchi Newspaper kwa kipindi cha miezi sita, na kuwapiga faini ya Tshs milioni 5.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya kubainika kuwa Aprili 13 kupitia mitandao ya kijamii Mwananchi Newspaper ilichapisha taarifa ya kupotosha kinyume cha Kanuni Na. 5(1)(a) na 12(l) za mawasiliano ya kieletroniki na posta, 2018

Mwananchi Newspaper waliitwa kujieleza kwanini wasifungiwe Aprili 15, na wakakiri kuwa kweli walikiuka kanuni hizo. Kwa kufuata sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Kifungu cha 28(1)(b) na (d) sura ya 172, ya mwaka 2017 wamepewa adhabu hizo

Iwapo Mwananchi Newspaper atashindwa kutekeleza adhabu hiyo TCRA itachukua hatua zaidi

Mwananchi.jpg

====
 

Attachments

Back
Top Bottom