Gazeti La Mwanaspoti: Muziki huu, utausoma kimya kimya

Gazeti La Mwanaspoti: Muziki huu, utausoma kimya kimya

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Hat trick zote
Yanga na Azam, licha ya kuwa na mastraika hatari zimeshindwa kushuhudia nyota wake yeyote akifunga mabao matatu ?hat trick? katika mchezo mmoja. Nyota wa Simba, Hamis Kiiza ?Diego? na Ibrahim Ajibu ndiyo pekee waliofanikiwa kufunga hat trick msimu huu na kuwapiku mastraika wengine zaidi ya 35 wa timu nyingine za Ligi Kuu.
Nyota hao wawili wanaifanya Simba itembee kifua mbele mtaani na kuwaponda watani zao Yanga kwamba licha ya kuwa na mastraika tishio kama Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Malimi Busungu bado timu yao imeshindwa kupata mfungaji yeyote wa hat trick.

Ufungaji
Ni kweli Simba ina uhaba wa washambuliaji ukilinganisha na Yanga na Azam, lakini cha kushangaza ni kwamba baada ya mechi tisa za msimu huu, Simba nayo imeweka mfungaji mmoja katika orodha ya wanaotisha kwa mabao msimu huu. Katika chati hiyo ya wafungaji bora mpaka sasa, nyota wa Simba Hamis Kiiza ?Diego? ni miongoni mwa wachezaji watatu waliofunga mabao manane msimu huu. Katika chati hiyo yupo pia Elius Maguli wa Stand United na Donald Ngoma wa Yanga.
Hata hivyo, Kiiza ndiye mwenye wastani mzuri zaidi wa mabao katika kila mechi kwani amecheza mechi saba pekee wakati Ngoma na Maguli wamecheza mechi tisa kila mmoja.

Ushindi mnono
Mabao 6-1? Ndiyo, kwani hujui kusoma namba? Alisikika shabiki mmoja wa Simba akimtambia mwenzie wa Yanga mtaani. Kejeli hiyo imekuja baada ya timu hiyo ya Msimbazi kuisambaratisha Majimaji ya Songea kwa mabao 6-1 juzi Jumamosi na kuwa timu pekee ya Ligi Kuu msimu huu iliyoweza kupata ushindi mkubwa zaidi. Simba imezipiku Yanga, Azam na Mtibwa Sugar ambazo ushindi wao mkubwa ni mabao 4-1 (Yanga na Mtibwa) na mabao 4-2 (Azam).
Ushindi huo unakuwa mkubwa zaidi kwa Simba tangu Agosti, 2013 ilipoifunga Mgambo JKT ya Tanga mabao 6-0 na nyota wa mchezo huo alikuwa Mrundi, Amissi Tambwe aliyetupia mabao manne.

Ulinzi imara
Simba inadaiwa kuwa safu mtepweto ya ulinzi msimu huu, lakini mpaka sasa ni miongoni mwa timu zilizoruhusu mabao machache zaidi msimu huu. Simba, Yanga, Azam (kabla ya mechi ya jana) na Mtibwa Sugar ndizo timu pekee zilizoruhusu mabao machache msimu huu na mpaka sasa kila moja imefungwa mabao matano. Mabao mengi zaidi Simba iliyoruhusu katika mchezo mmoja ni dhidi ya Yanga ambapo ilifungwa mawili.

Yaitega Yanga
Simba imecheza mechi nne ugenini mpaka sasa na kushinda tatu, ikipoteza moja na kujikusanya pointi tisa, wakati Yanga imecheza michezo mitatu mikoani na kushinda mara mbili na sare moja hivyo kukusanya pointi saba. Kitakwimu Simba inaonekana kuwa katika faida zaidi kwani Yanga italazimika kushinda mchezo huo mmoja wa ugenini ili kuipiku Simba katika pointi hizo, la sivyo itakuwa imeingia mkenge.
Pia Simba imefanikiwa kuvunja mwiko wa kutoshinda dhidi ya Mgambo JKT jijini Tanga na Mbeya City jijini Mbeya na katika mechi hizo mbili ilipata ushindi. Mabingwa hao mara 18 wa Ligi Kuu Bara, walikuwa hawajawahi kuifunga Mgambo jijini Tanga kwa kipindi cha miaka mitatu huku pia ikiwa wanyonge wa Mbeya City kwa miaka miwili mfululizo.

Source: mobile.mwanaspoti.co.tz/soka/Muziki-huu--utausoma-kimya-kimya/-/2481686/2939812/-/format/xhtml/-/4j67d6/-/index.html
 
nitashangaa sana simba wakimleta kavumbagu. Tunamuhitaji namba 10 n target man m1 mwingine. Simba tuna watoto the likes kina maganga. Sioni umuhimu wa kavumbagu.
 
Kama kuna mashindano yataanzishwa na TFF yakapewa jina Makapi Cup na tukaalikwa kushiriki.. Ubingwa utakua ni haki yetu.
hahaaha tusubiri tuone kama mtachukua kila kitu. Hiyo ndo itawafaa sana simba
 
nitashangaa sana simba wakimleta kavumbagu. Tunamuhitaji namba 10 n target man m1 mwingine. Simba tuna watoto the likes kina maganga. Sioni umuhimu wa kavumbagu.

Mkuu, ingawa kina Maganga, Ajibu, Kimwaga wako vizuri.. Tunamhitaji sana Kavumbagu.. Na hii ni kwa sababu..

1. Anaijua vizuri sana ligi ya Bongo.. So atasaidia sana ukuaji wa kina Maganga.. Na naimani kuwa na hawa madogo Kila siku watajifunza mengi saana.

2. Kavumbagu bado ni "mtamu" sana.. Japo Stewart Hall anampa Dk chache sana.. Ila akiingia tu lazima uone uwepo.. Katika mechi 2 za mwisho katupia goli 3.. Ni timu gani inaweza mkataa mchezaji kama huyu?
Pia katika misimu 3 iliyopita ameprove ubora wake.
 
Unamahaba -hasi mkuu sembo,pamoja na hat trick bado upo mkiani pyee pole

Mwandishi wa hiyo makala nilioibandika hapo juu.. alianza hivi..

WEKUNDU wa Msimbazi wanazidi kunoga, kiasi kwamba yale wanayofanya kwa sasa ni kama wanataka sifa na kutaka kuiletea kizaazaa Yanga. Juzi Jumamosi- waliifumua Majimaji ya Songea mabao 6-1 na kuwa timu pekee ya Ligi Kuu iliyopata ushindi mkubwa zaidi msimu huu. Wakati Yanga ndiyo timu yenye safu kali ya ushambuliaji,- haijafanya hivyo kwa msimu huu.

Japo mpo nafasi za juu.. Muwe tayari mda wowote kushuka chini.. Kwani mda si mrefu, tunarejea nafasi yetu tuliyokua kipindi tunamaliza ligi kwa staili ya kipekee kwa kumpiga mtani 5-0.
 
Sahau khs ilo jambo mkuu sembo,upinzani wenu mumemwachia azam
 
Sahau khs ilo jambo mkuu sembo,upinzani wenu mumemwachia azam

Kutetereka kwa mnyama ndani ya misimu 3 iliyopita.. Haiondoi ukali wake aingiapo mawindoni.

Kila napoulizwa unaiona wapi Simba S.C mwishoni mwa msimu huu??
Jibu langu hua ni jepesi.. Na wala sipepesi kabisa..
Namuona Mnyama akipeleka makombe haya mtaa wa Msimbazi..
1. Bingwa wa VPL msimu wa 2015/2016
2. Bingwa wa Kombe la Shirikisho a.k.a Azam Cup msimu wa 2015/2016
3. Bingwa wa Mtani Jembe 3
4. Bingwa wa Kombe la Mapinduzi mwaka 2016

Nina sababu zaidi ya Bilioni kuamini hivyo.. So mjiandae kufungasha virago.. Kwani Wenye Nyumba tushafika.
 
ni FARAJA mzuri, copy na share kwenye mitandao mbalimbali ili wanasimba wajifariji.
 
Back
Top Bottom