Gazeti la Nipashe: Posho za wafanyakazi ATCL ni kufuru, mabilioni yateketea

Gazeti la Nipashe: Posho za wafanyakazi ATCL ni kufuru, mabilioni yateketea

Kinuju

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2021
Posts
2,386
Reaction score
5,325
Habari.

Kwa wanaoshangaa wazo la waziri wa fedha Dr Mwigulu Nchemba la kuja na tozo kwenye miamala ya simu ili aweze kupata fedha za kukamilisha miradi ya kimaendeleo wanaombwa kusoma gazeti la nipashe la leo limekuja na ripoti maalum ya upotevu wa mabilioni ya fedha kwenye shirika la ndege la ATCL kupitia posho mbalimbali wanazolipana wafanyakazi!

Kwa maana nyingine kuna upotevu mkubwa wa kodi na mapato mbalimbali yanayokusanywa na serikali hivyo Mwigulu hana mbadala mwingine zaidi ya tozo ili akamilishe miradi yote.

20210725_094759.jpg
 
Shirika linajifia lakini bado wanalimalizia kabisa, Samia ageukie hapo atumbue watu aache kuwaonea huruma wasio na huruma na mali za umma, huu ukimya wake hii nchi itarudi enzi za shamba la bibi siku sio nyingi.
 
Habari.

Kwa wanaoshangaa wazo la waziri wa fedha Dr Mwigulu Nchemba la kuja na tozo kwenye miamala ya simu ili aweze kupata fedha za kukamilisha miradi ya kimaendeleo wanaombwa kusoma gazeti la nipashe la leo limekuja na ripoti maalum ya upotevu wa mabilioni ya fedha kwenye shirika la ndege la ATCL kupitia posho mbalimbali wanazolipana wafanyakazi!
Kwa maana nyingine kuna upotevu mkubwa wa kodi na mapato mbalimbali yanayokusanywa na serikali hivyo Mwigulu hana mbadala mwingine zaidi ya tozo ili akamilishe miradi yote.View attachment 1867358
Hilo si ndio shirika lenu pendwa ambalo hamkutaka likaguliwe, na wote waliojaribu kulisema vibaya mliwapa majina kibao ikiwemo kuwa wanatumiwa na mabeberu, waeneza ushoga na wanatumiwa na mabeberu?
 
Sitosahau ile siku Mwendazake aliyopokea gawio toka ATCL na kutuaminisha kuwa shirika linaingiza faida kumbe linaingiza hasara kwa miaka 5
Hizo wanazolipana posho ni bora wangetoa gawio .

Wanahitaji kubanwa tu
 
Wakishafuja pesa huko option pekee inabaki kuwakamua Wananchi kwa kisingizio cha uzalendo.

Kwa nini uzalendo usianzie kwao kwa kuacha wizi na ubadhirifu?

Hakuna hoja yoyote ya uzalendo bali ni matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya raia wa kawaida.
 
Kama kawaida watanzania wanafanyiwa spinning ya matukio kuwatoa kwenye suala la msingi.

Lengo ni kuwasahaulisha kuhusu tozo za ajabu ajabu
 
Back
Top Bottom