KUNA kila dalili kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ‘atasota’ rumande hadi kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania, Novemba 2025.
Lissu ambaye sasa amefunguliwa kesi ya uhaini, alikamatwa na Jeshi la Polisi Jumatano iliyopita - Aprili 9, 2025 katika Mtaa wa Soko Kuu, Wilaya ya Mbinga, Ruvuma baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.
Baada ya kukamatwa, usiku kiongozi huyo alisafirishwa hadi Dar es Salaam, ambako siku iliyofuata, Alhamisi – Aprili 10, alifikishwa Mahakama ya Kisutu, na kusomewa mashitaka ya uhaini na uchochezi.
Sheria za Tanzania zinaelekeza kuwa adhabu ya mtu anayepatikana na hatia kwa kutenda kosa la uhaini ni kunyongwa hadi kufa. Kesi zote zinazohusishwa na uhaini hazina dhamana nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche amesema alipata taarifa kutoka vyanzo vyake kuwa kukamatwa kwa Lissu kuna lengo aliloita baya; la “kumfungulia mashitaka ya uhaini.”
“Hawa watu wamejipanga kuzuia Chadema kuendelea na ajenda yake ya No reforms – No election, kwani wamegundua inakwenda kusimamisha uchaguzi, sasa njia ni moja – kumkamata Lissu na kumtia gerezani kwa muda mrefu, lakini nawaambia njama hiyo haitafanikiwa,” ameongeza Heche.
Heche anakituhumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupanga njama za kuhujumu Chadema ili kisiendelee na ajenda yake, kwa maelezo kuwa “ajenda yao imekishika pabaya” chama hicho tawala.
Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla alipoulizwa na Pambazuko endapo chama chake kinapanga njama dhidi ya Chadema alisema hawana nia ya kufanya hujuma kwa chama chochote cha upinzani, kwani CCM inapenda kushindana na vyama vyote kwenye sanduku la kura.
“Sisi tunapenda vyama vyote viingie kwenye uchaguzi na tuone wapigakura wanataka nani aongoze Tanzania kwa amani na kuleta maendeleo, hatuwezi kutamani chama chochote kutoshiriki uchaguzi,” alisisitiza Makalla.
Mwanazuoni mbobezi wa sayansi ya siasa, Dkt. Isaya Karsima, amesema kuwa kuna uwezekano kwamba kukamatwa kwa Lissu kunahusishwa na mahasimu wa chama chake, ambao wanaona kutokea kwa vurugu endapo kauli kali za kiongozi huyo hazitadhibitiwa.
Amesema moja ya njia za kunyamazisha sauti ya Lissu na msimamo wa chama chake ni kumkamata “mkubwa wao” na kuhakikisha anakuwa na muda mrefu ndani ya jela, na safari nyingi mahakamani hadi uchaguzi upite.
Muda wa kesi
Sababu nyingine ambayo iko wazi kuwa huenda Lissu akawa korokoroni (rumande) kwa muda mrefu ni muda wa kuendeshwa kwa kesi za uhaini.
Uzoefu unaonyesha kuwa kesi zote za tuhuma za uhaini nchini Tanzania – kama ilivyo maeneo mengi duniani, huchukua muda mrefu kufikia hukumu; iwe kuachiwa huru au kupata hukumu ya kifo au nafuu yake ambayo ni kifungo cha maisha haini nchini Tanzania hauko wazi au maalum kwa kila kesi, kwani unategemea mambo mbalimbali ikiwamo mambo haya yafuatayo; Uchunguzi wa awali; Uchunguzi wa Jeshi la Polisi na ushahidi wa upande wa mashtaka unaweza kuchukua muda mrefu, hasa kwa kesi kubwa na tata kama za uhaini.
Idadi ya washitakiwa na mashahidi; Ikiwa kuna washitakiwa au mashahidi wengi, kesi inaweza kuchukua muda mrefu zaidi. Rasilimali za mahakama; Upatikanaji wa
majaji, mawakili wa serikali, na miundombinu ya mahakama huathiri kasi ya usikilizaji wa kesi.
Rufaa au pingamizi; Kesi za uhaini mara nyingi hukumbwa na changamoto mbalimbali za kisheria, na kila hatua ya rufaa huongeza muda wa kumaliza kesi.
Upekee wa kosa la uhaini; Kesi za uhaini ni nadra Tanzania na hushughulikiwa kwa umakini mkubwa – na kuchukua muda mrefu, kwa sababu zinahusu usalama wa taifa.
Kesi za uhaini
Tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania, Desemba 9, 1961, Tanzania imekuwa na kesi mbili za uhaini ambazo zilifikishwa mahakamani na kutolewa hukumu.
Kesi ya kwanza ilianza kusomwa awali na baadaye mashikata Januari 19, 1970 ambapo washitakiwa zaidi ya 30 walikamatwa kwa kuhusishwa na njama za kutaka kumpindua Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.
Kesi hii ilidumu kwa miaka miwili, ambapo ilimalizika 1972 kwa baadhi ya washitakiwa kupewa adhabu ya kifungo cha maisha. Kesi nyingine – ya pili, ni ile iliyoanza Januari 28, 1984 na kumalizika Desemba 27, 1985, ambapo watu kadhaa walishitakiwa kwa makosa ya jaribio la kumuua Mwalimu Julius Nyerere na kupindua uongozi wake.
Historia inaonyesha kuwa kesi hizo maarufu zaidi zilihusisha madai ya majaribio ya mapinduzi yaliyokuwa yakihusisha wanajeshi, wanasiasa, wasomi na raia waliokuwa wakitaka “kuwepo kwa mabadiliko.”
Mwanasheria Obadia Msuya amelieleza Pambazuko kuwa historia inaonyesha kuwa hakuna kesi ya uhaini inayoendeshwa kwa muda mfupi.
Amesema kesi za uhaini huchukua muda mrefu, zingine hadi miaka mitano, kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo wepesi na utashi wa upande wa serikali kumaliza kesi mapema.
“Sioni maajabu yoyote kwa kesi hii ya uhaini dhidi ya Lissu ikimalizika mapema, huenda ikachukua muda mrefu zaidi, ukiwa mfupi sana, basi labda miaka miwili na nusu na siyo chini ya hapo...”
“Hizi kesi zina mambo mengi, kuna kuvutana kwa mawakili kuhusu tafsiri za sheria na mtazamo wa majaji, hii hufanya kesi kuchukua muda mrefu pamoja na mapingamizi ya hapa na pale, ngoja tuone mambo yatakavyokuwa, lakini hakuna namna ya kuifupisha kesi, labda ifutwe,” ameongeza mwanasheria huyo.
Hati ya mashtaka
Hati ya mashitaka dhidi ya Lissu iliyowasilishwa Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu inaonyesha kuwa kiongozi huyo wa chama cha upinzani, Chadema, anadaiwa kuwa kwa nia ovu ya uchochezi, alishawishi umma kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa 2025.
Wakili Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Nassoro Katuga, alieleza kuwa Lissu alitamka na kuandika maneno yanayohamasisha uasi.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga, Wakili Katuga akadai kuwa Lissu alitoa kauli zenye kuashiria uhaini ambazo ni pamoja na kauli hii; “Wakisema msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli..., kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi...
“Tutahamasisha uasi, hivyo ndivyo namna ya kupata mabadiliko..., kwa hiyo tunaenda kukinukisha..., sana sana huu uchaguzi tutaenda kuuvuruga kwelikweli..., tunaenda kukinukisha vibaya sana.”
Kauli hizo ambazo hati ya mashitaka inaonyesha zilitamkwa na Lissu ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam Aprili 3, 2025, ndizo zimetengeneza msingi wa shitaka la uhaini dhidi ya Lissu.
Lissu anashitakiwa chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, ambacho kinaeleza kuwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya uhaini atawajibika kwa adhabu ya kifo.
Hata hivyo, mahakama hiyo – ya Kisutu, haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhaini, na hivyo Lissu alirudishwa rumande hadi Aprili 24, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena. Mashauri ya uhaini husikilizwa Mahakama Kuu.
Ujasiri wa Lissu
Ulinzi mkali wa maofisa wa Jeshi la Polisi wakiwa na nguo za kiraia na wengine magwanda, walimsindikiza Lissu kuingia Mahakama ya Kisutu. Aliingia mahakamani saa 10:14 jioni.
Lissu hakuonekana kuwa na wasiwasi wala chembe ya taswira yenye kubeba woga, bali alionekana mtu aliyezoea korido na mazingira ya mahakama.
Nje na ndani ya mahakama hiyo, Lissu alionekana mwenye tabasamu na bashasha, kana kwamba ni “mume mtarajiwa anayesubiri mwanamwari wake.”
Muda mwingi alikuwa akinyanyua vidole viwili kutengeneza alama ya V, ambayo hutumiwa na Chadema kuonyesha ushindi.
Pamoja na uzito wa kosa lenyewe, lenye adhabu ya kifo, endapo atatiwa hatiani, Lissu alionekana kuwa na ujasiri – ambao watu wengi hawana.
Wakati kesi inaahirishwa, Lissu akiwa amevaa suti nyeusi aina ya Kaunda alisema; “kesi ya uhaini ni njia ya ukombozi.” Akiamini kuwa alichokisema “anasimama nacho na yuko tayari kukitetea.”
Mawakili wa Lissu
Katika kesi hiyo dhidi ya Lissu, tayari hadi juzi – Jumamosi, mawakili wanaofika 278 wa Tanzania na baadhi kutoka Zanzibar wameelezwa kujiandikisha tayari kumtetea Lissu mahakamani. Lissu ataletwa mbele ya mahakama hiyo Aprili 24, wakati kesi itakapoitwa.
Mawakili hao wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Dkt. Rugemeleza Nshalla, wataungana na wenzao ambao walikuwapo siku ya kwanza ya kuitwa kwa shauri hilo.
Hawa ni pamoja na Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gaston Garubindi na Michael Lugina. Peter Kibatala anatarajiwa kuungana nao.
Mbali na mawakili hao kutoka Tanzania, pia Lissu atakuwa akitetewa na jopo la mawakili kutoka Uingereza na Marekani kupitia Kampuni ya Amsterdam & Partners LLP; ambapo watatoa ushauri wa ziada wa kisheria kila utakapohitajika.
Dalili kukamatwa Lissu
Tangu kuanza kwa kampeni za kuipaza ajenda ya Chadema ya “No Reforms – No Election;” ya kuhimiza kuwepo kwa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi Tanzania, viongozi waandamizi wa chama hicho wamekuwa wakifanya mikutano mingi maeneo mbalimbali ya Tanzania kuelimisha umma juu ya ajenda hiyo.
Kundi kubwa la askari polisi wenye silaha kama ilivyokuwa Mbinga, hivyo “harufu” ya kutokea rabsha ilihisiwa mapema.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbless Lema, ambaye alikuwa eneo la tukio, alisema awali kuwa uwepo wa polisi wengi hakukuonyesha dalili njema, kwani tangu kuanza kwa ziara zao, hawakuwahi kushuhudia idadi kubwa ya askari wakiwa na silaha za kivita.
Akizungumza na Pambazuko katika eneo la tukio, Lema alisema; “kama hisia zilinituma kwamba katika mkutano huo, mambo hayatakuwa salama. Nilijua hatuwezi kumaliza salama hapa, na kweli yametokea. Inasikitisha sana haki na demokrasia kuharibiwa vibaya.”
Pambazuko lililokuwepo kwenye viwanja hivyo, lilibaini kuwepo kwa askari wenye magwanda na silaha wanaofikia 22, huku wengine tisa wakiwa wamevaa kiraia. Hawa baadhi yao pia walikuwa na silaha ndogo (pisto).
Sheria ya makosa ya uhaini Katika kulinda mamlaka na hadhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna sheria zinazolenga kuzuia matendo ya usaliti na uhaini dhidi ya serikali.
Sheria ya Uhaini Na. 2 ya mwaka 1970 imeweka bayana aina ya vitendo vinavyotafsiriwa kama uhaini na adhabu zinazofuata baada ya mtu au kikundi cha watu kubainika kutenda kosa/makosa ya uhaini.
Kwa mujibu wa Sura ya Saba ya sheria hiyo, mtu yeyote aliye ndani ya Jamhuri ya Muungano ambaye anapanga au kujaribu kumuua Rais wa Jamhuri, au kuanzisha vita dhidi ya taifa, anahesabiwa kuwa ametenda kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo.
Aidha, sheria hiyo inaainisha kuwa mtu yeyote anayesababisha au kusaidia kuondolewa madarakani kwa rais kwa njia isiyo halali, au kushiriki katika mipango ya mapinduzi, au kuchochea maandamano ya vurugu yenye lengo la kuipindua serikali, anahesabiwa kuwa ametenda kosa la uhaini.
Sheria hii pia inajumuisha wale wanaotenda njama kwa njia za siri au uwazi; ambapo pia matumizi ya propaganda au silaha ili kutishia amani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vivyo hivyo, mtu yeyote ambaye anashirikiana na adui wa taifa – awe ndani ama nje ya Tanzania, au anahamasisha matumizi ya silaha dhidi ya serikali halali, anahesabiwa kutenda kosa la usaliti au uhaini na adhabu yake ni kifo.
Sheria inamlenga pia mtu anayejaribu kulazimisha mabadiliko ya serikali kwa njia ya mabavu au vitisho kwa kuhamasisha kundi la watu kufanya uasi ambao lengo lake ni kuondoa serikali halali madarakani kwa njia zinazofurushwa na sheria.
Wadau wanena
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa, akizungumzia kesi ya uhaini dhidi ya Lissu amesema haamini endapo matamshi ya Lissu yanabeba uzito wa kosa la uhaini.
Olenurumwa amesema mashtaka hayo ni makubwa na yanakwenda kuweka dosari kubwa katika uchaguzi wa mwaka huu endapo ataendelea kushikiliwa.
“Uhaini ni kosa kubwa hapa nchini lisilokuwa na dhamana na lenye adhabu ya kifo au kifungo cha maisha. Ni kosa ambalo kwa miaka mingi sasa hapa nchini halijawahi kutumika pengine kutokana na uzito wake,”ameongeza.

JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.