Gazeti la The Citizen lahoji nani aliishauri Serikali kujenga SGR wakati wataalamu wanasema italeta hasara?

Tutaona jinsi kama wataweza kuendelea ku maintain hizo na kwenda na wakati zikiaanza kuchoka wabadilishe na kuleta mpya, pia kuhudumia hizo stesheni za marumaru, sio baadae vyoo vyote vimeziba na steshenii chafu na zimegeuka magofu...
DART yenyewe ni kichefuchefu muda huu...
Hapo ndio tutajua inaleta faida, lakini kwa bongo, the reality is the latter....
 
Huu ni ujinga wa Karne..Huwa wanajenga kumnufaisha mjukuu gani?

Nyumba sio reli,reli inaenda na teknolojia ya wakati huo Ili ilete faida sio kusubiria ,ukisubiria teknolojia inapita inakuwa chuma chakavu.
Wach uwongo bwana; reli ni msingi na mataruma yake. Kitakachobadilika na teknologia ni vichwa na mabegewa lakini msingi na mataruma havibadiliki. Trans Siberia ya Urusi ilianza kujengwa mwaka 1891 na kufunguliwa mwaka 1904 yaani takriban miaka 120 iliyopita na bado inadunda leo. Unadhani gharama zilizotumika kujenga reli ile mwaka huo wa 1891 kwa leo zitajenga umbali gani kama siyo asilimia tano tu.

Wewe na mwandishi wa makala hiyo ni kama mchumia njaa ambaye anafanya kazi ili apate chakula cha siku hiyo hiyo, hamuangalii mbali zaidi ya leo na kesho.
 
Tatizo letu linabaki palepale watu weusi tuna shida sana na wanaoweza kuwa wanahoji hv ni walewale watu weusi wenzetu wanaotumika kila kukicha kama majini ya kishetani kwanza tusidhani kila anayehoji SGR ana akili timamu usidhani Kila mtu atakusifu ukifanya vzr si rahisi kamwe hao wanao hoji SGR hawajielewi wanapaswa kutambua kwamba Ulimwengu umekwenda mbali sana hivyo hatuwezi baki nyuma kiasi hicho.
 
Kwa nini reli za TAZARA na kati zimeshindwa kuendeshwa kwa ufanisi?

Kama hizo zilizokuwa za kawaida ilishindikana kuendeshwa kwa ufanisi kwa nini tuamini hii nyingine zitaendeshwa kwa ufanisi ?
 
Tumeshindwa kuendesha BRT kwa faida, tutaweza endesha SGR? Ni ndoto za alinacha tu. Huo mradi utatugharimu pakubwa, tena bora hata kama reli ingeelekezwa Songwe, lakini nako TAZARA ni siasa iliyotushinda.
 
Hilo ndilo swali muhimu linalotaka jibu.
Jinsi ya kuboresha uendeshaji; na wala siyo ujenzi wa reli ya kisasa.
Kwa nini reli za TAZARA na kati zimeshindwa kuendeshwa kwa ufanisi?

Kama hizo zilizokuwa za kawaida ilishindikana kuendeshwa kwa ufanisi kwa nini tuamini hii nyingine zitaendeshwa kwa ufanisi ?
Swala la uendeshaji ni tofauti kabisa na uhitaji wa reli mpya ya kisasa.

Ukitaka kulijadili hilo unakaribishwa.
 
Mwacheni Mungu aitwe Mungu !! Wanayaona yote yanayowatokea wao na wenzao lakini bado hawataki kujirekebisha na kutubu !! Ni ajabu sana !! Pesa haziwezi kuwaletea peace of mind pesa haiwezi kuwaletea Afya njema Bali Ni Mungu pekee ndiye awezaye kukupa hayo yote mema !! Nashangaa kwanini hawataki kuamini Hivyo !! Au ndio La kuvunda halina Ubani !!
 
Tumeshindwa kuendesha BRT kwa faida, tutaweza endesha SGR? Ni ndoto za alinacha tu. Huo mradi utatugharimu pakubwa, tena bora hata kama reli ingeelekezwa Songwe, lakini nako TAZARA ni siasa iliyotushinda.
Kwani miaka yote watakuwepo hao hao wabadhirifu wa mali za Umma ??!!
 
Kwani Hangaya anasemaje!?
Huyu alikuwa rubani msaidizi enzi hizo.
Na alishasema miradi yote iliyoanzishwa itaendelezwa! Tusubiri tuone kampeni chafu za wenye malori na mabasi kama zitafanikiwa! Maana inasemekana wanasiasa wengi ndio wamiliki wa hiyo kazi !! Mungu anawaona !!!
 
Aliyewaambia SGR ilijengwa kuleta faida ni nani? Hii imejengwa kutoa service kwa wananchi na faida watapata walipa kodi...ndiyo maana miradi ya aina hii wati binafsi wanaikimbia
Pia itatusaidia barabara yetu kuu ya kati itabaki salama kwa miaka mingi sana !!
 
Jibu hoja badala ya kuja na vimaneno vya jumla jumla vya mtu asiye na ubongo..


Gazeti limesema.wazi akili za hivi ndio zinasanabisha Afrika kuwa maskini mile maana itafika wakati tunaanza tena kutumia Kodi kulea mamiradi hewa tuliyotumia matilioni kuyajenga.
 
Of course nilikutana nazo,kila mwenye akili timamu anaelewa tumepigwa na kitu kizito kichwani..

Yaani tumeongeza mzigo mwingine kwa walipa Kodi kwamba mashirika mengine yanayotutia hasara hatujaridhika nayo tukaongeza na hili..

Aisee natamani wahusika wanyongwe.
 
Wakati inaanza kujengwa mlisema hawatoweza,baada ya kuiona inajaribiwa mnaanza italeta hasara hamueleweki nyie minyoo jike humohumo dume humohumo.
 
Wakati inaanza kujengwa mlisema hawatoweza,baada ya kuiona inajaribiwa mnaanza italeta hasara hamueleweki nyie minyoo jike humohumo dume humohumo.
Sio kuweza swala ni tija,sgr sio pambo 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220722-185451_Twitter.jpg
    30.2 KB · Views: 5
Mleta mada ungeweka article kama ilivyo bila tafsiri yako, wengi waliojibu wasingekuwa na cha kusema kwa kushindwa kuelewa kinachozungumziwa na mwandishi. Hoja ya kiuchumi ijibiwe kiuchumi sio vihoja vya mabeberu, mbona nchi zao wamefanya, wivu wa Kenya kwetu na mengine kama hayo
 
Jadili hoja kwa hoja sio kuropoka matusi..

Matusi hayajibu hoja..

Swali jingine Kati ya Mwanza na Tunduma wapi sgr ilitakiwa kuelekea kwa kuzingatia maslahi ya Taifa na Takwimu [emoji116]?
Unataka Jiji la Mwanza na kijiji Cha tunduma afu unaonyesha mizigo ya kwenda nchi zingine!! Onyesha mizigo ya Mwanza vs Tunduma ndo utaona wapi reli ilipaswa kuelekea, aliyekudanganya hii reli tunajengewa wananchi wa nchi zingine ni nani?! Yaani mwananchi wa Zambia apate bidhaa kwa bei nafuu iliyosafirishwa kwa gharama nafuu kupitia reli ya watanzania iliyojengwa Kodi za watanzania, afu muda huo huo mtanzania wa Dodoma, tabora, singida, shinyanga, Mwanza,nk apate bidhaa kwa bei mbaya huku akiwajengea wazambia SGR?! Huo ni upuuzi. Hii reli inajengwa na watanzania kwa ajili ya watanzania wala sio kwa ajili ya hao wacongo wako.
 
Naona kuna kitu kwenye hoja hii ingawa siwezi kusema zaidi kwani sijaona source yake hiyo na kujisomea mwenyewe. Pili naangalia tulichojifunza kwenye TAZARA reli iliyojengwa miaka ya sabini, inavyosuasua pamoja na kuhudumiwa na serikali mbili bado ni shida kubwa. Reli hii ni ya kawaida sana haina technologia ya juu na nishati kama SGR tunayoijenga. Bado management aspect ya uendeshaji wa SGR tunayoijenga achilia mbali mizigo inayotarajiwa kusafirishwa na reli hiyo ya SGR. Reli hii imepelekwa Mwanza kwanza badala ya Kongo, Burundi and Rwanda au Uganda sioni cha kusafirishwa kutoka mwanza, kilimo cha pamba kimekufa, abiria sioni. may be some cargo to Uganda through lake Victoria hadi Port Bell in Uganda ( Port-Bell Uganda wanamifumo ya wagons za train za zamani need to be ungraded). Kinachotia shaka kidogo ni technolojia itakayotumika kama umeme, tukumbuke hizi ni fast trains, management aspect of it. Sisemi tusijenge tulipofikia ni point of no return why it will be more expensive. Ku-break even hili ni swala jingine sometimes investment nyingine ni geopolitical nature, and Regional-economic factors. Chelewa chelewa unakuta mwenzio ameshachukua wateja wote. Natarajia mradi huu kuhudumiwa na serikali kwa muda mrefu kufikia break even point huu ndio ukweli.
 
Hoja yakoni ya kisiasa zaidi sio kiuchumi. Hatuwezi kujenga SGR kwa kuangalia soko la ndani tu, basi sisi ni wendawazimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…