Gazeti la The Citizen lahoji nani aliishauri Serikali kujenga SGR wakati wataalamu wanasema italeta hasara?

Tena hilo LI sgr ndio limejaa siasa..

Kwa Takwimu hizi hapa sgr itapata wapi mzigo wa kubeba Ili isiwe siasa? 👇
Kuhusu hizo takwimu, nadhani hakuna haja ya kuwa na woga katika hilo kwani uchumi wa nchi hizi siyo STATIC, yaani siyo USIOKUA, bali ni uchumi dynamic, endelevu na unaongezeka with time. Hivyo suala la huo mzigo lisiwe hoja wala kigezo cha kutuzuia kujenga SGRs katika nchi zetu; hata hao huko majuu walipokuwa wakijenga hizo SGRs zao walikuwa na economic growth projections. Tuliangalie suala hili KICHANYA zaidi kuliko KIHASI zaidi. By the way hizo data ni za LINI, yaani za MIAKA GANI?
 
Hao wataalamu mbona huwa hatuwaoni kwenye vipindi vya television wakiongelea hizo hasara kwann wanaongelea kwenye vichochoro huko wakitegemea sisi tuwaelewe mbwa hao.
 
Wazungu wanajua kila watachosema tutakiamini haraka sana bila hata kuja na hitimisho la tafiti zetu.

Rejea maelekezo yao kipindi cha Coronavirus pandemic kutoka kwao wakasema idadi ya watu watakao kufa African countries itakuwa mara dufu ya ile ya ulaya. Nini kilitokea tulipopuuza takwimu zao mbwa wale?!

Leo tena mnawasikiliza kuhusu maswala yetu ya kiuchumi?! Hii reli ni yetu sisi na ndio tutakaopangia matumizi. Biashara na mazingira ya kiuchumi kila siku yanabadilika. Wao wanaweza dhania tutasafirisha watu tukabadilisha tukaanza kusafirisha mizigo.

Sisi ndio tutajua cha kufanya sio wao watuambie cha kufikiria au kufanya juu ya maisha yetu na mazingira yetu mbwa hao.
 
Kama hata historua hujui wewe ni cheti feki..

Hakukenga kwa kutoa huduma Wala kujifurahisha bali kusafirisha mali ghafi kwa faida na walifanya hivyo uzalishaji wao ulipokoma na reli zilikoma kuleta faida hadi kesho.
Kwani matumizi ya reli ni yale yale tu. Hatuwezi badili Matumizi kulingana na uhitaji?!

Nitakupa mfano mwakyembe alikuja na idea nzuri ya kubadili matumizi ya vichwa vya treni ambavyo vililala tu havina kazi muda wa asubuhi hadi usiku.

Uliona impact yake ?! Kiwango cha pesa kilichokuwa kinapatikana?!

Sasa wewe na hawa wazungu wako matako yao kuja kutupangia matumizi ya rasilimali zetu as if sisi bila wao hatuwezi ni ujinga na kukosa akili kiwango cha juu sana.

Hiyo reli wacha ijengwe na inafaida sana na uchumi wetu ikisimamiwa kiusahihi kuna mambo mengi yatafunguka hapo ni swala la muda na jitihada.
 
Soma hiyoo [emoji116]
Kwahiyo wakishindwa wao na sisi tutashindwa kwasababu wao na sisi tunafanana kila kitu?!

Hii ndio changamoto ya wasomi wa Tanzania na afrika. Kila kitu mzungu akisema hakiwezekani na nyie mnaunga nyuma kama madereva wa IST wameunga nyuma ya ambulance.

Acheni hizi fikra potofu za kuamini kila anachosema mzungu. Taarifa zake unatakiwa uzitumie kuchukua tahadhali tu ila sio kufanyia maamuzi ya mwisho.

Mnaboa sana watu wa namna hii yaani kwa mzungu mnakuwa kama mke kwa mume wake mnatii kila kitu anachosema bila kuhoji.
 
Soma hiyoo [emoji116]
Kwahiyo wakishindwa wao na sisi tutashindwa kwasababu wao na sisi tunafanana kila kitu?!

Hii ndio changamoto ya wasomi wa Tanzania na afrika. Kila kitu mzungu akisema hakiwezekani na nyie mnaunga nyuma kama madereva wa IST wameunga nyuma ya ambulance.

Acheni hizi fikra potofu za kuamini kila anachosema mzungu. Taarifa zake unatakiwa uzitumie kuchukua tahadhali tu ila sio kufanyia maamuzi ya mwisho.

Mnaboa sana watu wa namna hii yaani kwa mzungu mnakuwa kama mke kwa mume wake mnatii kila kitu anachosema bila kuhoji.
 
Unaongozwa na woga
Ni zaidi ya uoga na ujinga juu. Sasa watu kama hawa ndio wamejazwa katika taasisi za serikali na mawizarani huko waoga wa kufanya maamuzi magumu yatayo wanufaisha raia.

Wao ni kuogopa ogopa tu na kusikiliza wazungu wanasemaje kila siku. Hawapo serious na maamuzi au fikra zao ni kuogopa ogopa tu takataka kabisa.
 
Mh.. uchumi wa nchi hizi Tz, Kenya, etc umeganda kama barafu.. uchumi wa South per capita income ya South Korea mwaka 1961 ilikuwa around 500USD.. leo hii ni close to 45,000USD..
linganisha na wetu sasa, kati ya 1961 na 2020 umeongezeka kwa ngapi? labda 700USD..
Sasa ni uchumi upi unaosema uko dynamic?

Weka propaganda pembeni ongea facts
 
Uoga ni nini?.. kwa nini wataalam na viongozi wanaogopa kufanya maamuzi?
Sababu: kwenye mambo ya maslahi ya umma haupaswi kukosea kwa sababu unaweza ukafungwa kwa sababu ya makosa hayo.. wwtu hawatadhani ilikuwa bahati mbaya bali ilikuwa maksudi na kwa maslahi binafsi.. kwa hiyo mtu anayeongoza ofisi ya umma sharti asikosee..

Kwa nini uoga wa kufanya maamuzi? Kwa sababu maamuzi mengi kibongo bongo yanafanyika bila information/data za kutosha kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kufanya makosa katika mazingingira kama hayo..

Na imani elimu hii itakuwa ya manufaa kwako ili usiwe unafoka foka tu.. kulaumu watu kushindwa kufanya maamuzi.
Maamuzi katika mazingira ya Tz mtego sana ndo maana watu wanaona bora wasifanye maamuzi
 
Reli iliyojengwa na mkoloni ushakula matunda yake au bado?
Tumekula sana tu kwa kusafiria ndani yake! Huduma zake zilikuwa nzuri sana kipindi kile tulikuwa tukipewa warranty kusafiria kwenda mashuleni na kurudi majumbani kwetu wakati wa likizo!! Zamani ukiambiwa elimu bure ujue ni bure kweli mpaka usafiri unalipiwa !! Huduma za reli zimekuja kuharibika baada ya watu kubadilika na kuanza kujilimbikizia mali!! Hiyo mentality ya watu kuanza kufikiria kujilimbikizia mali ndiyo iliyoleta shida zote zilizopo nchini mpaka leo na kesho pia zitaendelea kuwepo !! Sgr ijengwe tu kuliko pesa kuachiwa watu wenye fikra za kujilimbikizia mimali !!
 
Naomba mtusaidie sisi wagumu kuelewa!

Hivi ukiwa unaishi Kigoma, ukatumia SRG kwenda Dar kwa masaa kadhaa, ukafanya mishe zako halafu ukarudi siku hiyo hiyo Kigoma, je, hiyo siyo faida?

Upo Dodoma, unaenda Dar chap na kurudi na kuendelea na mishe zako, hiyo siyo faida?

Au faida ni lazima ubebe mizigo mingi kwa pamoja?
 
Are you saying uchumi wa nchi zetu haukui!? Siyo kweli! Uchumi wa nchi zetu unakua ndio maana hata ukienda kwenye statistics zako, utaona kuwa per capita income ya nchi zetu ya mwaka 1961 hadi 2000 (uno quote) siyo sawasawa na ya leo! Uchumi wetu unakua ila siyo kama wa hiyo nchi unayosema. Chumi hazilingani ndio maana nchi nyingine zinajitangaza MUFILISI!
 
Mshua alikua na kauli yake ukiongea pumba anakwambia "BOX KABISA"
 
WAZUNGU: Msichimbe Bwawa la Stiglers mnaharibu mazingira

WAZUNGU: Msijenge Standard Gauge railway mtapata hasara.

POPOMA MMOJA: Wamesema tusijenge Standard Gauge tutapata hasara

MAPOPOMA WENGINE: Clap clap clap
 
Kulipasikana kubadilisha SGR iwe ni Dar-Dodoma-Tunduma! SGR kwenda kanda ya ziwa au Kigoma si mambo sahihi.

Any transport professional angeangalia freight growth na ukweli haiko mshariki ya Congo, bali kusini ya Congo (inayohudumia Kinshasa) na Zambia!! Dar-Dom ingeunganishwa na treni ya kasi lakini pia mizigo mingi ingewahi kufika!! Kufa kwa TRC na TAZARA yalikuwa ni makosa makubwa. Natumaini tutakuwa tumepata funzo!

Financing option haikuwa ya kisasa! Mismanagement kiwango cha TRC kitatusikitisha sana. Ufanisi kiwango cha TRC itakuwa ni kifo, kama financing option ingekuwa PPP - huenda private sector ambayo haivumilii hasara ingeleta jambo la kuifundisha TRC ili reli yao iende sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…