Gazeti la The Citizen limeupotosha umma kuhusu hisa za Vodacom

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
Gazeti la The Citzen linapaswa kupuuzwa kwa kile ilichofanya kuandika kuwa kampuni ya Vodacom inapanga kuomba kuongezewa muda wa kuuza hisa zake kuwaruhusu wageni kununua hisa za Vodacom.

Huku ikichukua mfano kutoka kwa wakala mmoja ambaye ni Orbit Securities aliyeidhinishwa katika ukusanyaji wa awali wakisema ameshindwa kufika lengo walipanga kuuza hisa za bilioni 200 lakini mpaka sasa wameuza hisa za bilioni 150. Je kuuza robo tatu ya hisa kwa wakala mmoja aliyeidhinishwa ni kushindwa kufika lengo?

Kampuni ya Voda waliwaidhinisha mawakala zaidi ya 14 katika uuzaji wa hisa zenye thamani inayakadiriwa kufika bilioni 476 ambazo Vodacom wanatarajia kuzikusanya.

Mawakala wa ukusanyaji wapo 14 projection ya wakala mmoja haitoi Picha kamili ya biashara jinsi ilivyofanyika kwanini mwandishi wa gazeti la the Citzen asisubirie taarifa za mwisho kutoka kampuni husika wakatoa idadi ya jumla ya idadi ya hisa zilizouzwa?

Shares za Vodacom nilizifuatilia. Kupitia prospectus yao nikaisoma. Presentation ya financial statements zao za mwaka 2016 na projections ya 2017 na 2018 zinavutia sana kulinganisha na kampuni nyingine zinazofana na Vodacom.
Annual revenue yao ni kubwa around bilioni 900 mpaka 1trillion.
kwa short term wakiweza kuziuza hisa baada tu ya IPO kufungwa kuna uwezekano wa price kupanda juu na hii pia inategemeana na hali ya uchumi wa nchi.
Ingawa kupanda pia kwa bei kunaweza kuwa kwa kiwango kidogo na hii itategemeana na hali ya uchumi wa nchi.

Na sera ya gawio ipo wazi kabisa baada ya Faida asilimia 50 baada ya kukatwa kodi kwa mwaka na Gawio litakwenda kwa kila mwanahisa wa kampuni.
Mfano unamiliki hisa 100 na kampuni imegawa labda shingi 5 kwa kila hisa ni 100 x 5= 500

IPO bado muda wake kumalizika mwisho ni tarehe 19 Mwezi huu wa Nne vodacom watatupatia mrejesho.

Kwa rational investor ukifanya mahesabu utaona kwamba investment kwenye Vodacom ni best choice kwa current financials na projections ya 2017 na 2018. nimefanya share performance ratios nimeliona hilo.

Karibuni [HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG]
 
Mkuu naona umetoa povu sana.

Kwa rational passive investor pekee ndio anaweza kushadadia hayo unayosema
 
Magazeti mengi ni wamepotoka na kushindwa kubalance Story
Wamekuwa kama Magazeti ya Udaku yanayoandika habari mbaya tu za wasanii.
 
Mkuu naona umetoa povu sana.

Kwa rational passive investor pekee ndio anaweza kushadadia hayo unayosema
Gazeti hili limepotoka Kwa habari za Uongo [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Dkt Maguful naye alifute tu hakuna namna.
Maana haiwezekani watu wanaojitoa katika kile kinachotakiwa na rais waandikwe vibaya kiasi hiko.
Ina maana gazeti hilo limeshindwa kuandika kwamba Vodacom ndio kampuni ya simu Tanzania iliyo ingia ktk soko la hisa?
 
Mnyonge mnyongeeni ila haki yake mpeni,....... Vodacom Tanzania wamejitahidi kwa hili sasa kila Mtanzania anaweza kununua hisa kwa bei rahisi ambayo sawa na bure.....
 
Mnyonge mnyongeeni ila haki yake mpeni,....... Vodacom Tanzania wamejitahidi kwa hili sasa kila Mtanzania anaweza kununua hisa kwa bei rahisi ambayo sawa na bure.....
Vodacom kiukweli ndio mtandao bora kabisa nchini kwetu,umewanufaisha wengi sana kiuchumi na watu wengi bado wanautegemea kama kitega uchumi chao.tuwapongeze kwa kweli wamejitaidi sana.
 
Wekeza Vodacom, the great manipulators, at your own risk.
 
Maisahau kuwaambia wenye hisa kuwa ili wa-break even kwa hilo gawio la sh 50 kwa hisa ya 850 watahitaji miaka 17!!

Sasa kama sio ukichaa ni nini? Na hapo faida inazidi kupungua kutokana na strong competition.
 
Mlikuwa wapi kupiga debe mpaka muda wa kuuza hisa umeisha? Mmejifungia maofisini badala ya kukuta mitandaoni mujibu hoja,sasa fursa ya kujibu hoja iko hapa JF,ombeni muda uongezwe na nyinyi muuelimishe umma

Na Vodacom ni sehemu ya wadhamini wa JF,itendeeni haki kampuni yenu
 
Hii ni aibu kwako mleta hoja. Unataka kusema wewe huelewi kuwa Orbit Securities ndiye anayeruhusiwa kukusanya taarifa za mawakala wote nchi nzima na hivyo anachokisema yeye kinatokana na kile alichokikusanya kwa mawakala wote wanaohusika ktk zoezi la kuuza hisa za Vodacom? Sijawahi kuwa na wasiwasi na uwezo wa gazeti la The Citizen katika kuandika habari za aina hii na pengine hujafuatilia hili zoezi na jinsi walivyoli-ripoti hao jamaa na ukakimbilia kuleta hoja ili kukidhi mahitaji yako ya PR. Umepotosha vibaya mtoa hoja mpaka umewafanya baadhi ya wachangiaji watoke nje ya mada kabisa.
 
Wewe mleta mada ndiyo hukuelewa kilichoandikwa. Undersubscription ni wawekezaji kutochangamkia hisa zote zinazouzwa. Sababu inawezakuwa kwa sasa hivi kuna ukata mkubwa Sana. Hivyo ni wachache wana uwezo wa kununua hizo hisa za Vodacom. Orbit Securities hawakukosea kutoa taarifa. Ingawa na wao ni brokers lakini wao ndiyo main collectors wa IPO ya Vodacom. Mawakala wengine wanawasilisha kwao. Hivyo wao ndiyo wenye picha kamili ya mauzo/makusanyo.
 
Magazeti mengi ni wamepotoka na kushindwa kubalance Story
Wamekuwa kama Magazeti ya Udaku yanayoandika habari mbaya tu za wasanii.
Msiwalaumu sana "The Citizen" kwani wao wenyewe Chanzo chao cha hiyo taarifa ni jarida la Kimarekani " BloomBerg"
 
Voda spn mashine imeanza, shares za voda at 850 wamezoverprice na watu wamelionaa hilo. Tarehe 19 sio mbali tutaona ukweli.
 
Mfano
Kama wanaongeza iyo Tsh 5. Asilimia ngapi? Wanakata makato ya kodi ya serikali. Kama wanakata asilimia 14%. Apo inakuwa angalau afadhali lakini wakikata zaidi ya asilimia iyo inakuwa ishu ngumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…