Gazeti la The Economist laandika; "Is Samia Suluhu Hassan Africa's most dissappointing president?"

Gazeti la The Economist laandika; "Is Samia Suluhu Hassan Africa's most dissappointing president?"

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Gazeti la The Economist la Aprili 30, 2026 limechapisha makala yenye kichwa: "Is Samia Suluhu Hassan Africa's most disappointing president?" — yaani "Je, Samia Suluhu Hassan ndiye rais aliyekatisha tamaa zaidi barani Afrika?"

1777616515463.png

Katika makala hiyo, The Economist inaelezea Ukatili wa dola, likisema Tanzania inakabiliwa na ukatili wa dola, na "scores" yaani makumi ya viongozi wa upinzani wamepotea.

LinagusiaVurugu za uchaguzi 2025 likisema baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025, kulikuwa na maandamano makubwa.

Ripoti za UN zinasema vikosi vya usalama viliua mamia ya watu, vikawaacha wengi kujeruhiwa na kukamata maelfu. Watu wanadai risasi za moto zilitumika dhidi ya raia. Amnesty International inataka serikali ichapishe ripoti ya uchunguzi kuhusu vifo 518 vilivyotokea baada ya uchaguzi huo.
Pia gazeti hilo linaeleza kuhusu ukandamizaji wa upinzani, ambapo viongozi wa upinzani na wanaharakati wamekamatwa.

Waangalizi wa Jmoja wa Afrika walisema uchaguzi haukuwa wa kuaminika na walibaini kujazwa kwa masanduku ya kura.

Kwa upande mwingine, Gazeti la Daily News la Tanzania liliandika, The Economist imeikosea Tanzania.
Gazeti hilo limeeleza kuwa Samia si rais wa kidikteta, bali anaongoza nchi katika "kipindi kigumu cha mabadiliko" chenye mafanikio ya kiuchumi, ushirikiano mpya na dunia, na hatua za uwajibikaji. Mwendesha boda aliyenukuliwa alisema: "Tunataka amani zaidi".

Hata hivyo, awali Samia mwenyewe alikiri kuwa "picha mbaya tuliyojitengenezea" baada ya uchaguzi inaweza kupunguza uwezo wa Tanzania kupata mikopo.

Awali alisifiwa kwa kufungua nafasi ya kisiasa, lakini wachambuzi sasa wanasema uongozi wake umegeuka kuwa wa kimabavu.

Soma zaidi: https://www.economist.com/leaders/2...ointing-president?utm_campaign=shared_article
 
The answer is YES.SAMIA is disappointing president because she killed half of all tanganyikans for its unacceptable election
 
Nendeni mkawajibu 'Yes" mumfurahishe lissu na kitima Kisha rudini makwenu mkalime.

Mama yupo busy anaijenga nchi. Daraja la jangwani Lina zaidi ya 40% Sasa.
 
Back
Top Bottom