Times: Hamas imeihadaa Israel, kama Muhammad Ali Clay alivyomfanya Foreman
Gazeti la Uingereza la "The Times" limeandika kuwa Israel itaondoka katika vita vyake dhidi ya Gaza ikiwa dhaifu baada ya kuangukia katika mtego ule ule uliowatumbukiza Wamagharibi kwenye vita vya Iraq, na kuondoka kwenye vita hivyo wakiwa wamechoka zaidi na kuwa hatarini zaidi, sambamba na kupoteza mamlaka yao ya kimaadili.
Katika makala iliyoandikwa na Matthew Syed, gazeti hilo limeanza kwa kuzungumzia stratejia iliyotumiwa na bondia Muhammad Ali Clay dhidi ya mpinzani wake, George Foreman, katika pambano lao la kihistoria mwaka 1974, ambapo alimkasirisha mpinzani huyo kwa kejeli, hivyo akajibu na kujichosha. Foreman anakumbuka kwamba Muhammad Ali alimwambia, "Je, hayo tu ndiyo uliyo nayo, George?" The Times limeandika kuwa bondia George Foreman alijipiga ngumi katika hali ya uchovu, na Muhammad Ali akamtoa nje katika raundi ya nane.
Mwandishi amelinganisha mkakati huu na kile kilichotokea baada ya matukio ya Septemba 11, 2001, wakati viongozi wa Marekani na Uingereza walipoamini kwamba uvamizi mkubwa dhidi ya Afghanistan na Iraqi ungewafanya kuwa salama zaidi, lakini walikuwa katika makosa; na walifanya mashambulizi makubwa na kuua mamia ya maelfu raia. Gazeti hilo limesema: Wamagharibi walirudi kwao wakiwa wamechoka zaidi na kukabiliwa na hatari kubwa zaidi, wakiwa wamepoteza mamlaka yao ya kimaadili, kama mpinzani wao, Al-Qaeda, alivyotaka.
Tiimes limeripoti kuwa, Israel imetumbukia katika mtego uleule na kwamba "Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilifuata mkakati wa hali ya juu zaidi, katika kuitia hamaki Israel kwa Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa tarehe Oktoba mwaka jana.
Mwandishi wa gazeti hilo la Uingereza amehitimisha kwa kusema: Mpango uliobuniwa kwa umakini mkubwa wa kuitia hamaki Tel Aviv umeifanya Hamas kuwa na nguvu zaidi na kuiweka Israel katika nafasi dhaifu.
Amesema mashambulizi ya Israel dhidi watu wa Gaza, uharibifu mkubwa na mauaji ya raia yamedhihirisha umwagaji damu mkubwa wa utawala huo na kuifanya Israel itengwe zaidi katika Umoja wa Mataifa kiasi kwamba, hata washirika wake wanaanza kufikiria kuiwekea vikwazo.