Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Leo gazeti la RAI linalomilikiwa na mwizi wa Sh bilioni 40/- kutoka EPA, Rostam Aziz limemtukana Dr Slaa na kumuita kila majina machafu – udini, umbumbumbu, ulaghai etc.
Mtakumbuka Rostam anakingwa na JK katika tuhuma hizo ambazo hela zilizoibiwa ndiyo zilimuingiza madarakani mwaka 2005.
Hadi sasa Rostam hajakamatwa kushitakiwa, mojawapo ya kitendo ambacho ndicho kinachosababisha JK kukataliwa na wananchi, ambao wanaona rais huyo amesalimisha mamlaka yake yote kwa kikundi cha mafisadi wachache wa kihindi huku akicheka cheka na kuonyesha meno.