GDP ya nchi inapimwa kwa Mtaji wa fedha au jumla ya mali zote zilizopo nchini kwa maana ya majengo, ardhi, rasilimali nk

Jojo123

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2013
Posts
432
Reaction score
703
Habari wanaJf

Week hii tunaona IMf iki isifia Tanzania kupaa kiuchumi kutoka 69.9bilion Dollar kwa Miaka miwili tumefikia 85.45Bilion dollar.

Ambapo wastani wa pato la mtu moja moja ni sawa na Dollar 1320$, ingawa sijui hii wastani una angaliwa kwa Mwezi au kwa mwaka.?

Sasa swali langu ni je! hii GDP ya dolar bilion 85.45 sawa na Trillion 200 Tsh.

Je hii thaman kuu inajumlishwa kutoka katika mali zote za nchi, au mtaji wa fedha zilizopo katika mzunguko wakila siku. Au wana piga hesabu ya rasilimali za nchi zote, ndio wana pata kama zikiwekwa sokoni ndio inapatikana jumla ya thaman kuwa ikiuzwa na kugawanywa kila mtu ata pata kiasi cha dollar 1320$

Naombeni anaye jua kuelezea hii GDP inapatikanje anisaidie?

Natanguliza Shukranj.
Asanten.
image_ab7090a9-d0a2-488c-9878-480c4332b2fd20230422_111103.jpg
 
GDP inapimwa kwa kuhesabu thamani ya bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi husika kwa kipindi fulani cha wakati (kawaida mwaka mmoja)...

Thamani ya bidhaa na huduma hizo huweza kupimwa kwa kutumia mtaji wa fedha, yaani thamani ya pesa ambayo imetumiwa kuzalisha bidhaa na huduma hizo...

Kwa hiyo, GDP inaweza kuwa kipimo cha thamani ya uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa kutumia mtaji wa fedha...

Hata hivyo, GDP pia inaweza kuwa kipimo cha thamani ya uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa kutumia jumla ya malighafi na rasilimali zinazopatikana ndani ya nchi husika, ikiwa ni pamoja na majengo, aridhi, na rasilimali nyingine...

Hii ni kwa sababu rasilimali hizo pia hutumiwa kuzalisha bidhaa na huduma, na kwa hiyo zinachangia kwa jumla ya thamani ya uzalishaji...
 
Nimekusoma.. sasa najiuliza wanajuaje idadi ya majengo yote nchini na bei zake au bidhaa zote ili hali kuna wazalishaji wadogo ndani ndani hawaonyeshi mahesabu yao TRA wala wala takwimu ya makazi haikuwa ikichukuliwa kujua dhaman ya majengo inchini
 
Kujua idadi ya majengo yote nchini na bei zake ni kazi ngumu na inahitaji utafiti wa kina na makini...
Kwa hiyo, serikali hukusanya data na takwimu za kiuchumi kwa kutumia mbinu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na sensa za watu na makazi, sensa za viwanda na biashara, na tafiti mbalimbali za kiuchumi...

Mamlaka ya Takwimu Tanzania, ndiyo yenye jukumu la kukusanya na kuchapisha takwimu rasmi za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na takwimu za idadi ya majengo na bei zake...

Ili kupata taarifa sahihi kuhusu idadi ya majengo na bei zake, utafiti wa kina hufanywa kwa kuuliza wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi na nyumba...
Hii inaweza kuhusisha tafiti za kitaalamu na mahojiano na wataalamu wa ujenzi, wamiliki wa majengo, na wengineo...

TRA, wanaweza kupata taarifa za kodi za majengo na nyumba kutoka kwa wamiliki wa majengo na nyumba, ambazo zinaweza kutumiwa kutoa takwimu na taarifa kuhusu thamani ya majengo na nyumba...
 
duh.. haya
GDP ni thamani ya ya bei ya sokoni ya bidhaa na huduma ambayo nchi imezalisha kwenye kipindi Fulani mara nyingi mwaka mmoja.

Huwa kuna vitu kama vinne hutumika kupima.
GDP = c+I+G+(x-m)

C=consumption(kiwango cha matumizi ya watu Kwa bidhaa zilizozalishwa ndani).
I=investment (uwekezaji)

G=government expenditure on final goods or service mf, mishahara, ujenzi WA Barbara nk

X-m=tofauti ya bidhaa mlizouza nje, na bidhaa mlizoagiza kutoka nje.

Taarifa nyingi za GDP huwa ni makadirio, hakuna survey inayoweza kutembelea kila MTU na kumuuliza kiwango alichozalisha na alichonunua kwenye kila kona ya nchi husika.

Kama nchi ikifanikiwa na uwezo kufanya consumptions kubwa basi GDP yake itakuwa kubwa mfano ni USA

Import ikiwa kubwa kuliko export hiyo nchi lazima inaweza kuwa na uchumi WA kusua sua.

GDP ina changamoto nyingi, ukuaji wake unaweza ukawa unachangiwa na watu wachache ama sekta chache ambazo hazigusi watu wengi.

Kwa mfano ukuaji WA GDP WA Tanzania WA sasa umechangiwa Sana na sekta ya huduma hasa utalii baada ya COVID. Utalii haugusi watu wengi kama kilimo au manufacturing industry. Matokeo yake ni Kwamba unaambiwa kuwa uchumi umekuwa lakini watu wakiangalia hali ya maisha imezidi kuwa ngumu.

Kwa sababu ni sekta chache Sana na zinazogusa watu wachache ndio zilizochangia hiyo GDP mwisho WA siku income inequality. Changamoto ya uchumi unaotegemea huduma huwa unajikita Sana mijini na hata uwekezaji WA serikali umekuwa unafanyika mijini zaidi. Wakati huo asilimia kubwa ya watu wapo vijijini

Mbaya zaidi manufacturing industry TZ ni kama haipo nchi ina-import Sana bidhaa toka nje kuliko kuexport, si rahisi kuexport huduma,
 
Asante sana nimekuelewa sana..
 
Uandishi wako mbovu kabisa. Nitakurekebisha kwa ku bold maneno uliyokosea.
Habari wanaJf

Week hii tunaona IMf iki isifia Tanzania kupaa kiuchumi kutoka 69.9bilion Dollar kwa Miaka miwili tumefikia 85.45Bilion dollar.

Ambapo wastani wa pato la mtu moja moja ni sawa na Dollar 1320$, ingawa sijui hii wastani una angaliwa kwa Mwezi au kwa mwaka.?

Sasa swali langu ni je! hii GDP ya dolar bilion 85.45 sawa na Trillion 200 Tsh.

Je hii thaman kuu inajumlishwa kutoka katika mali zote za nchi, au mtaji wa fedha zilizopo katika mzunguko wakila siku. Au wana piga hesabu ya rasilimali za nchi zote, ndio wana pata kama zikiwekwa sokoni ndio inapatikana jumla ya thaman kuwa ikiuzwa na kugawanywa kila mtu ata pata kiasi cha dollar 1320$

Naombeni anaye jua kuelezea hii GDP inapatikanje anisaidie?

Natanguliza Shukranj.
Asanten.View attachment 2596257
Screenshot_20230424-034213_Chrome.jpg
 
Uandishi wako mbovu kabisa. Nitakurekebisha kwa ku bold maneno uliyokosea.

View attachment 2597603
Kama concept ime eleweka na wanao stahiki kunijibu maswali yangu na wamesha nijibu.. wewe unaye kuja kukosoa swali usha chelewa na nisha pata majibu kwa walio nielewa.. je wewe unataka kunijibu issue za sarufi na mantiki kwani ndio lengo langu?
 
Ni ushauri tu, boresha your writing skills
 
Kama concept ime eleweka na wanao stahiki kunijibu maswali yangu na wamesha nijibu.. wewe unaye kuja kukosoa swali usha chelewa na nisha pata majibu kwa walio nielewa.. je wewe unataka kunijibu issue za sarufi na mantiki kwani ndio lengo langu?
 
Je, mizunguko ya pesa katika mabenki haiakisi hali ya uchumi wa nchi ?
 
badala ya ku select embu rewrite upya nijue kosa langu ndugu
 
Back
Top Bottom