Geez Mabovu ameacha deni kwa vituo vya redio, kucheza nyimbo zake sasa hazililipi

msafwa93

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
4,786
Reaction score
5,963
Geez Mabovu amefariki katika kipindi ambacho kwa asilimia kubwa alikuwa amepotea kwenye masikio ya wengi. Na mara nyingi sababu za kupotea kwenye masikio ya watu ni kutochezwa kwa nyimbo za msanii katika vituo vya redio.



Kwahiyo haimaanishi kuwa kupotea kwa msanii kwenye masikio ya watu kunatokana na ukimya wake mwenyewe bali ni kutopata nafasi ya nyimbo zake kuchezwa kwenye vituo vya redio zaidi hata kwenye TV.

Mara ya mwisho kukutana na Geez Mabovu na kuongea naye ilikuwa January 7 mwaka huu pale Msasani Club kwenye kilinge. Nilizungumza naye kwa kirefu na alikuwa mengi ya kueleza kutokana na kupotea kwake. Pamoja na wengi kutomsikia, Geez alikuwa akiendelea na harakati zake za kuachia ngoma.

Sauti yake nzito na uandishi wa akili ulikuwa bado uko vile vile. Siku za hivi karibuni afya yake ilikuwa imedhoofika kiasi pengine ni kutokana na kunywa sana pombe kali. Lakini hiyo haikuwa imeathiri uwezo wake wa pekee katika kuandika na kuchana.

Geez uliyemsikia kwenye ngoma zilizohit kama ‘Mtoto wa Kiume’ ‘Mimi’ na zingine ndiye yule yule aliyesikika kwenye wimbo wa hivi karibuni ‘U Can’t Stop Me Now’ aliomshirikisha Joh Makini na Nisher.

Huu ni miongoni mwa nyimbo za hip hop zilizotoka miaka miwili iliyopita na bora kabisa. Bahati mbaya wimbo huu haukupata nafasi na mashabiki wengi wa hip hop hawakupewa haki ya kuusikiliza. Pengine ulikuwa na nafasi kubwa ya kumrejesha tena kwenye chart. Iwapo wimbo mkali kama huo ulinyimwa nafasi, msanii arekodi wimbo wa aina gani ili apewe fursa? Hatuoni kama kuna tatizo sehemu? Tatizo ambalo linatakiwa kurekebishwa.

Redio hazikuutendea haki wimbo huo. Redio hazikumtendea haki Geez Mabovu. Redio zina deni kubwa kwa Geez Mabovu. Bahati mbaya deni hilo haliwezi kulipwa sasa. “Tulipofanya hii ngoma kwa Majani nikamwambia ‘Geez hii ngoma kali’ lakini mimi ndiye niliyekuwa namcheck sababu nilikuwa naiona ile ngoma,” amesema Joh Makini.

“Nilikuwa nahisi kuna matatizo yanamsumbua au labda ni life au stress whatever. Nilikuwa nikiuangalia huo muziki niliofanya na yeye na nikiulinganisha na muziki wa hip hop uliopo kwenye mainstream, nilikuwa naona muziki mkubwa sana ndio maana nilikuwa namuambia niachie huu muziki uwe wangu ili niupush wewe uwe kama umeshirikishwa.”

Haisadii tena kucheza nyimbo zake sasa hivi labda kama lengo ni kumuenzi, lakini si kwa kumsaidia yeye kuishi. Geez hatuko naye tena. Geez hahitaji tena show.



Redio hazikitakiwi kukumbuka kucheza nyimbo za wasanii wenye vipaji kama hawa wakifariki, haiwasaidii, inawaletea huzuni tu ndugu na mashabiki wake.
Sikumbuki ni lini katika miaka mitano iliyopita Geez Mabovu alitajwa kutumbuiza kwenye show yoyote kubwa. Mtu kama huyu ambaye anatagemea muziki anaishi vipi? Roma aliandika jambo la msingi na lenye ukweli kuwa hakuna watu wenye stress kama wasanii.

Kuna vipaji vingi vinapuuzwa sasa. Tunasubiri vipotee kabisa ndio tuanze kucheza nyimbo zao? “Wasanii kama Geez Mabovu tunao wengi sana hapa ‪Tanzania lakini hatujifunzi kwa mifano,” anasema Roma.

“Kuna vipaji havipaswi kupuuziwa hata kidogo jamani vipeni support, hundred please. Hatatokea msanii kama ‪ Afande Sele‬, mi nakwambia hadi leo ni mkali sana huyu mtu. Hakuna rapper‬ kama ‪Jos Mtambo‬ asikwambie mtu. Yule ‎Enika‬ yule ni anaimba jamani acha tu. Hawa vijana wa ‪‎Tamaduni Music‬ ni new ‪‎faces‬ zinazokuja vizuri sana wapewe ‪‎support ‎Joslin‬, MB Dog, hawa watu ni ‪Almasi‬ jamani. Tuna wasanii wakali kibao mi nakwambia ‪‎Dojo na Kaya ni ‎ny**o. Wataimba wote ila mtu kama ‪ Rama Dee‬ ni hadithi nyingine ujue,” anasisitiza.

“Wito wangu tafadhali tuwasapoti na tuzidi kuwasapoti vijana wetu wenye vipaji,” Roma anatoa ushauri. “Najua wapo wenye matatizo lakini tusiikate tamaa tuzidi kuwaonyesha njia bora ya mafanikio.”

Nilizungumza na Joh Makini ambaye ameshawahi kufanya ngoma zaidi ya tatu na Geez Mabovu na wana historia ndefu naye. Joh anaamini kuwa hakitatokea kizazi cha muziki wa hip hop bora kama chao na hivyo kukipuuza ni kosa kubwa. “Hofu yangu ni kwamba industry ya hiphop itachukua muda sana kupata generation kama hii. Na pengine inaweza isitokee tena,” anasema Joh.

“Hicho kipaji cha Geez Mabovu, Ngwair, Langa, Joh Makini, Nako 2 Nako, Fid Q, Mapacha, sidhani katika miaka miwili ijayo tutakuwa na kizazi kama hicho. Tukiwa nacho pia tutakuwa tumebarikiwa,” anasisitiza rapper huyo ambaye yeye na wenzake Weusi waliamua kuahirisha show yao ya Mbeya wiki hii kwa heshima ya Geez.

Ngwair, Langa na Geez Mabovu wamefariki katika kipindi ambacho vyombo vya habari vilikuwa vimewapa mgongo. Kosa hili litaendelea kutokea kama tutashindwa kuvienzi vipaji vilivyopo sasa.

Badala ya kuanza kulaumiana katika kipindi ambacho maji yameshamwagika na hatuwezi tena kuyazoa, tujifunze kutokana na makosa na tuvipe nafasi vipaji vinavyostahili kupewa.

IMENAKILIWA KUTOKA::BONGO5.com
 
The other side of the coin huwa haizungumzwi,mwenye ujasiri akijitokeza atarushiwa chupa za mikojo,mawe,atatukanwa,(yalimtokea ommy dimpoz aliposema kuhusu ngwair),jamaa yetu(RIP)alikuwa ni mlevi sugu hasa wa spirits kuhusu ngoma(unga)sidhani kama aliwahi kutumia lakini ulevi sugu nao umechangia sana kifo chake also katika hekaheka zake to 2000's hajaweza hata kujiwekeza hata kidogo kwa kufungua kimradi chochote kidogo(just a question) tukishamaliza kuongelea mazuri kama hayo hapo kwenye uzi tuangalie na makosa waliyofanya ndugu zetu waliotangulia mbele za haki ili wasanii na wengine tusio wasanii tujifunze kuwa you must choose to LIVE or to PERISH through our actions
 
R.i.p wana hiphop wote mlio tutangulia clouds hata mkifa wote siwezi kuwa lilia mna watnyonya na kuwatumia wasanii kisha mna wapotezea,furaha yenu ni kuona wasanii wanafulia au mnapenda kujiona Miungu watu tuje kuwalilia? chid benz na wewe kaa chini tulia dili za unga sio ishu usije ukatokomea ooh my God ninayo mengi ya kuongea ila sema tu bundle lime niishia.
 

Naelwa sana what u feel mkuu. Ila Mungu ndo atawafuta machozi wanyonge.
 
Kuna tatizo ambalo linaogopwa kusemwa pia ambalo ni poor management ya wasanii wengi hasa wa Hip Hop wakipata nafasi ya kuchomoza wanatoka kwenye uhalisia wa utamaduni wa Hip Hop na kuanza kuiga maisha ya wasanii wa nje kwa 100%(ulevi,umalaya,tattoos,dharau etc)na hakuna wa kuwaongoza na wengi wao wanaenda kama wehu na kila mafanikio yanavyoongezeka ndio kichaa kinazidi zaidi,ivi mbona wakiwa kwenye peak hawafanyi jambo la msingi la kuwaletea maendeleo pale ambapo watashuka siamini kua akili zao zinawatuma kua on the top milele.
Media power ina mchango mdogo sana kwa kadhia inayowakumba wasanii wetu ila tumeamua kuwatupia lawama zote ili kuficha mapungufu ya wasanii nakumbuka Geez aliwahi kupata show na akalipwa vizuri lakini akabaki mkoani anazitapanya zile pesa mpaka akakosa nauli ya kurudi Dar na bado tunawalaumu watu wa media ivi ni mara ngapi wasanii tunaowajua tunakutana nao wakiomba misaada ya kijinga kama vocha,nauli na bia wakati hela zao wamewekeza kwenye starehe na mavazi na ufike wakati tujiulize aya magari,cheni na mavazi ya gharama wanayotuonyesha kwenye mitandao ya kijamii wakiamua kuwekeza sehemu naamini hii neno "natumia unga,pombe na bangi cuz nna stress "litaisha otherwise kuna foleni ndefu sana na bado lawama zitakuja kwa shetani Media.
Rest In Peace Meddy 'Pengo' Upete i'm sure there's Heaven for O'Gz.
 
Mnatoa Lawama za bure kwa media! Muda mwingine nyie mashabiki ndio chanzo cha nyimbo zao kutochezwa maana mnazisifia kwenye mitandao halafu kwenye maradio hamziombi!

Na mnatakiwa kujua muda mwingine media haziwezi cheza wimbo ambao hauombwi! Wanatoa kulingana na mahitaji ya wateja!
 
"kutaka kujua ukweli ni sawa na kumenya kitunguu kila ganda litakutoa machozi" by fid Q
 

we Acha Kuwachuria Clouds
Kwani Wao Pekee Ndio Wanaredio Hapa Town?
Hao Wasanii Wangekuwa Na Akil Si Wangefungua Radio Yao
Wasanii 100 Wakijipanga Vizuri , Wanatosha Kuwa Na Redio Kubwa Zaidi Ya Mawingu!
 
nakumbuka kuna wakati nilikuwa na geez kino b kuna bar moja hivi tunapiga toli,akaniambia dah diamond katoka mbaya"zamani dogo alikuwa ana chana"
kitambo diamond aliomba kufanya naye truck ya rap
goma linaitwa "jisachi"
 
tatizo ni uwezo mdogo wa kufikiri wa hao wanaoitwa wasanii. hela wanapata jamani, hizi milioni kumi, kumitano haziwapigi chenga. kwanini hawawekezi kwenye biashara? najua wengi mtadai wametengwa na baadhi ya media, lakini vipi kuhusu lady jaydee amabaye nae kuna baadhi ya media zimemtenga? mbona anafanya vema na hatujaskia anabwia unga kwa kisingizio cha stress? wasanii hasa nyie wa Hiphop acheni kuiga maisha msiyoyajua
 
nakumbuka kuna wakati nilikuwa na geez kino b kuna bar moja hivi tunapiga toli,akaniambia dah diamond katoka mbaya"zamani dogo alikuwa ana chana"
kitambo diamond aliomba kufanya naye truck ya rap
goma linaitwa "jisachi"

Ile trak ni nyoko zipo m2 tatu ngwair(rip),Geez(rip) na Domo.

“Jisaaachiii kabla mfuko haujatobokaa full msimbazi kama adili wa choka"
 

Hii tabia ya kukaririshwa story za mwaka 47 inabidi kuepukana nazo kabisa. We nchi nzima ina Radio zaidi ya 80 sasa iweje kila lawama mnairushia media moja? Kwani clouds ndo wanazuia nyimbo zisichezwe kwenye media nyingine? Kama media zote zikicheza nyimbo zake kutoa clouds unataka kusema msanii hawezi kusikika??? Hizi lawama nyingine ni upuuzi mtupu na kadri mnavyozidi kuwaombea vibaya wao ndo wanazidi kupasua anga kwasababu maombi yenu yapo wrong.

Mashabiki mnayo nafasi yenu ya kumtoa msanii. Kila media inavyo vipindi vya mashabiki kuomba nyimbo lakini hamziombi. Na media zinaendaga na upepo wa mashabiki unavyoenda. Kama hasikiki ina maana watanzania hawajamkubali hata media haiwezi kumng'ang'ania. Kumkubali kwako haimaanishi ni mkali kwa watanzania wote.

Naamini alikuwa hakubaliki ki hivyo kama mnavyotaka kutulazimisha.
 
poor management wanajisahau a
wakijua siku zote watakua kwenue peak
 
nakumbuka kuna wakati nilikuwa na geez kino b kuna bar moja hivi tunapiga toli,akaniambia dah diamond katoka mbaya"zamani dogo alikuwa ana chana"
kitambo diamond aliomba kufanya naye truck ya rap
goma linaitwa "jisachi"

Mkuu ulikuwa naye mitaa ya Aika nini.Unajua Marehemu angekuwa teja lakini alikuwa kila akivuta poda anatoka majipu usoni maana yake ulimkataa.R.I.P Med Pengo.
 

Unazijua FIGISUFIGISU za OSATA? OSATA ndio Clouds FM ikiongozwa na Ruge huku washambuliaji ni Othman suka SAid fela na TAle Babu.
 
Mtakuaga mnasingiziaa na radio za buree jamaniii,,,,angeimba vizurii radio zingeicheza hata bila ye kutaka,ila vipaji vya kulazimisha ndo hivyooi
Mauti ni lazimaa kwa binadam hata ukwepejeee,,sema sie binaadam hatujitunzi ndio maana tunakufa haraka
 
Mbona Jide nyimbo zake hazipigwi Clouds na hakuna lililomkuta?

ruta jide mi namkubali lakini sijui km atakuwa yule tena maana historia sio kivile km yahaya na zingine labda huu mpya anaotarajiwa kutoa
 
Watu tumezidi kuleteana lawama zisizo na msingi majibu mafupi ni haya ukweli ni kwamba hip hop haiuzi bongo fleva ni muziki wa entertainment..muziki unapendwa na wengi unlike hizo hip hop ambazo watu wa huko mikoani mnazi embrace kwa namna moja au nyingine kwani mtu huwezi kua na mitazamo ya ki-hip hop halafu ukafanya bongo fleva? hizi habari za kujifanya sijui mwana harakati blah blah kala pina yuko wapi? diamond alikua anarap mr blu nae hivyo hivyo lakini wakaacha wakaanza kuimba maisha sasa hivi ni pouwa kiaina..unaweza nikosoa pale ambapo nimeenda out of point...
 
System ya kuomba nymbo haitumik ckuhzi..
Ona pale claudz kpnd cha xxl n cha masaa ma3 lakin nymbo za kuombwa znazopgwa n 3 tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…