Geita: Ajali ya basi la Sheraton yaua 7 na kujeruhi baadhi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Watu saba wamefariki dunia na wengine ambao idadi bado haijajulikana kujeruhiwa katika ajali ya gari la Sheraton lililopinduka baada ya tairi la mbele kuchomoka na kuangukia mtaroni, wakati likitokea mkoani Mwanza kwenda Ushirombo wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Ajali hiyo imetokea leo Machi 7, 2023 imetokea majira ya saa10:30 jioni katika Kijiji cha Mwilima karibu na mbuga ya Ibanda mpakani mwa mkoa wa Geita na Mwanza.

20230307_214906.jpg

====

Watu saba (7) wamefariki dunia huku wengine wakijeruhiwa katika ajali ya basi la abiria kampuni ya Sheraton lenye namba za usajili T922 ADC iliyokuwa ikitokea Jijini Mwanza kuelekea Lunzewe Wilaya ya Bukombe ajali ambayo imetokea kwenye mtaa wa Mwilima kata ya Kanyara mkoani Geita.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Amesema, ajali imetokea leo Machi 7, 2023 majira ya saa 10:30 jioni na kueleza chanzo cha ajali ni kupasuka kwa tairi ya mbele ya basi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Martine Shigela amefika kwenye Hospital ya Rufaa Mkoani humo kwa lengo la kuwajulia hali majeruhi ambapo ameagiza kwa Jeshi la Polisi ni vyema likafanya ukaguzi wa mara kwa mara pindi Magari ya abiria yanapotokea Pointi A kwenda Pointi B.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita ambapo majeruhi walipelekwa katika kituo cha Afya Kasamwa kwa huduma ya kwanza na kisha hospitali ya rufaa ya mkoa kwa matibabu zaidi.

Chanzo: Jambo TV
 
View attachment 2540997

Duuh hii tofauti na Ile ya mpanda ? hatari sana 16 lost lives today
 
Naona askari wa usalama barabarani hawapo kazini kweli kweli wanaendelea kula bata kwa kwenda mbele

Haiwezekani kila kukicha ajali sipati pkcha wakagi wa magu haikuwa hivi tulisahau kama kunatokeaga ajali

Mpaka asikari walikuwa wanajisifu kwamba wamepunguza ajali kwa asilimia 70 mbana sasa hivi hakuna nini kinajili mungu atusaidie tutaisha naogopa hata kusafiri
 
Wameondoka barabarani kuwaondoleeni usumbufu.
 
Hili basi nmelipanda Adubuhi jana tu kutoka ushirombo kwenda katoro jamaani mmmh

Pumuzikeni kwa amani[emoji120]
 
Watakuja kushtuka tunaongoza kwa ajali barabarani duniani kote harafu tutaema kale ka usemi tunaupiga mwingi
 
Back
Top Bottom