Geita: Auawa akidaiwa kujaribu kumbaka mwanafunzi

Kaka yangu ni mlemavu wa akili (down's syndrome) jumapili alichomwa moto akiwa mzima hadi kufa walidhani ni mwizi ukimuangalia vizuri unamjua kabisa huyu ni tahaira.
Lakini cha ajabu waliofanya tukio ilo wameachiwa huru wapo uraiani licha ya kuwepo ushaidi wa video
 
Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 18 hadi 22 ameuawa na mwili wake kuchomwa moto na wananchi wakidai kuwa alijaribu kutaka kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili katika Sekondari iliyopo Kata ya Bombambili mjini Geita.

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi Februari 24, 2022 saa 12.30 asubuhi wakati mwanafunzi huyo akiwa njiani kwenda shule.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa mwanafunzi huyo alitoka nyumbani alfajiri kuwahi shuleni na akiwa njiani ndipo alipokamatwa na kijana huyo akimvutia kichakani kwa lengo la kumbaka.

β€œAlipomkamata mwanafunzi alipiga kelele na wananchi walikusanyika na kumzingira. Walianza kumuokoa mwanafunzi na kumpeleka shule kisha kumshambulia kijana huyo hadi kumuua na mwili wake kuchomwa moto,” amesema Kamanda Mwaibambe.

Kufuatia tukio hilo, Mwenyekiti wa mtaa huo Salum Maige anashikiliwa na Polisi kusaidia kufahamika kwa wote waliohusika kwenye mauji hayo.

β€œMarehemu alishazingirwa hatuoni sababu za kumuua zaidi ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria. Kwa kuwa mauaji yamefanywa na wananchi wa eneo hilo tunamshikilia mwenyekiti ili asaidie polisi kuwapata wahusika,” ameongeza.

Chanzo: MWANANCHI
 
Mwenyekiti anaonewa. Labda kama na yeye alikuwepo kutekeleza mauwaji hayo
 
Sasa kati ya wewe uliyeua na huyu aliyetaka kubaka, wapi ilipo dhambi kuu!! Huu ni utoto tu na huwenda walikubaliana kiutoto na wakakubaliana kuamka mapema
 
Pole sana kwa kuondokewa na Kaka yako, hapo hilo suala lifikishe juu zaidi kwa waziri na IGP na humu humu jukwaani endelea kulisema hili naamini litafanyiwa kazi.
 
Geita mbona hamcheki mbona hamuongei?

Mmmmh Geita pa moto mweeh[emoji848]
 
Na huyo mwanafunzi akamatwe asije kua alikula hela ya nauli.



Ova..
 
Kuna uwezekano Mwenyekiti ili kujinusulu anaweza akataja watu ambao hawakuwepo au akataja ambao alikua na ugomvi nao.. Hawa polisi wetu wa hovyo kweli kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…