Geita: Chuo Kikuu cha Utumishi wa Umma kujenga Kampasi yake Wilayani Chato

Geita: Chuo Kikuu cha Utumishi wa Umma kujenga Kampasi yake Wilayani Chato

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la kanda ya ziwa kitajengwa wilayani Chato, amethibitisha waziri wa utumishi wa umma George Mkuchika.

Kwa mujibu wa Mkuchika ni kuwa amejiridhisha kuwa Chato inazo sifa zote zinazoiwezesha kujenga chuo hicho ikiwemo ukubwa wa eneo unaoridhisha.

=======

TPSC KUJENGA KAMPASI CHATO KUKIDHI KIU KANDA YA ZIWA

CHUO cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kiko mbioni kujenga kampasi wilayani Chato, mkoani Geita itakayotoa fursa ya mafunzo kwa Watumishi wa Umma na wananchi wa Kanda ya Ziwa.

Akikagua eneo litakalojengwa Kampasi hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni mstaafu George Mkuchika alisema ameridhika na eneo lililotengwa kwani ni rafiki kwa usalama na utoaji wa elimu.

Kampasi itajengwa eneo la Rubambangwe lenye ekari 41.66 na itahudumia mikoa ya Geita, Mwanza, Kagera, Shinyanga, Simiyu na Mara.

Waziri Mkuchika alisema Kanda ya Ziwa pekee ndiyo ilikuwa haijabahatika kuwa na Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma, hivyo fursa hii ni muafaka na itakuwa na manufaa kwa watumishi wa umma na wakazi wa eneo la Kanda hiyo.

Akizungumzia uamuzi wa kujenga Kampasi hiyo wilayani Chato, Mkuchika alifafanua kuwa halmashauri ya wilaya ya Chato imetoa kiwanja hicho bure tofauti na maeneo mengine ya Kanda ya Ziwa ambayo yangekigharimu chuo fedha nyingi kununua kiwanja.

Aliishukuru halmashauri kwa kutoa kiwanja na kumhimiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa hati kwani chuo kiko tayari kuanza ujenzi mapema iwezekavyo.

Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dk Emmanuel Shindika aliwathibitishia wakazi wa Kanda ya Ziwa kuwa fedha za kuanza ujenzi zimeshapatikana, hivyo kinachosubirikiwa ni hati.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Medard Kalemani alimtaka Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo kuwasilisha maombi ya kupatiwa umeme katika eneo hilo ili kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa kampasi hiyo.

Akizungumzia eneo ambalo chuo kitajengwa, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel alisema ujenzi wa kampasi hiyo ukikamilika itakuwa ni chachu ya maendeleo kutokana na muingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali watakaokuja kupata mafunzo na utavutia uwekezaji.
 
Chuo kikubwa cha utumishi wa umma tawi la kanda ya ziwa kitajengwa wilayani Chato, amethibitisha waziri wa utumishi wa umma George Mkuchika.

Kwa mujibu wa Mkuchika ni kuwa amejiridhisha kuwa Chato inazo sifa zote zinazoiwezesha kujenga chuo hicho ikiwemo ukubwa wa eneo unaoridhisha.
Aiseeeee.

Shobo na Uchawa on Freak.
 
Chuo kikubwa cha utumishi wa umma tawi la kanda ya ziwa kitajengwa wilayani Chato, amethibitisha waziri wa utumishi wa umma George Mkuchika.

Kwa mujibu wa Mkuchika ni kuwa amejiridhisha kuwa Chato inazo sifa zote zinazoiwezesha kujenga chuo hicho ikiwemo ukubwa wa eneo unaoridhisha.
Afadhari, Dar kwenyewe kumejaaaa!
 
wataalamu wa mambo wanakwambia, huko napo ni tanzania...kwahiyo kunafaa kupelekewa sio tuu bandari ya kisasa...hata beach kidimbwi nayo ipelekwe huko
 
477510958.jpg
 
Hongera kwake Mkuchika. Chato ni Tanzania na chuo ni cha watanzania
 
Chuo kikubwa cha utumishi wa umma tawi la kanda ya ziwa kitajengwa wilayani Chato, amethibitisha waziri wa utumishi wa umma George Mkuchika.

Kwa mujibu wa Mkuchika ni kuwa amejiridhisha kuwa Chato inazo sifa zote zinazoiwezesha kujenga chuo hicho ikiwemo ukubwa wa eneo unaoridhisha.
MAMBO ya ajabu Sana haya.Hata speaker marehemu SAMUEL SITA enzi za uhai wake akiwa alipokuwa speaker wa bunge,alijenga ukumbi wa bunge na ofisi ZAKE za kifahari huko kwao URAMBO.Mpaka leo Hakuna hata mkutano mmoja TU wa bunge ambao umeshafanyika kwenye huo ukumbi.
 
Back
Top Bottom