Trillion
JF-Expert Member
- Apr 24, 2018
- 3,330
- 7,494
Si ndio, wanatekekeleza kwa kishindo,Wacha weeee !!!
Nchi ya chama kimoja.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si ndio, wanatekekeleza kwa kishindo,Wacha weeee !!!
Yes!Serikali isijenge tawi la chuo cha utumishi wa umma - kama inataka kuwasaidia watu ijenge tawi la chuo cha SUA (umuhimu wa kada hii ktk maendeleo ya kilimo ni mkubwa sana hasa kuchochea ukuaji wa sekta binafsi, uchumi, uwekezaji na huduma za kitafiti kwa wakulima)
Tusiharibu fedha za umma
Sitashangaa, ule Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ukihamishiwa Chato...Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la kanda ya ziwa kitajengwa wilayani Chato, amethibitisha waziri wa utumishi wa umma George Mkuchika.
Kwa mujibu wa Mkuchika ni kuwa amejiridhisha kuwa Chato inazo sifa zote zinazoiwezesha kujenga chuo hicho ikiwemo ukubwa wa eneo unaoridhisha.
=======
TPSC KUJENGA KAMPASI CHATO KUKIDHI KIU KANDA YA ZIWA
CHUO cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kiko mbioni kujenga kampasi wilayani Chato, mkoani Geita itakayotoa fursa ya mafunzo kwa Watumishi wa Umma na wananchi wa Kanda ya Ziwa.
Akikagua eneo litakalojengwa Kampasi hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni mstaafu George Mkuchika alisema ameridhika na eneo lililotengwa kwani ni rafiki kwa usalama na utoaji wa elimu.
Kampasi itajengwa eneo la Rubambangwe lenye ekari 41.66 na itahudumia mikoa ya Geita, Mwanza, Kagera, Shinyanga, Simiyu na Mara.
Waziri Mkuchika alisema Kanda ya Ziwa pekee ndiyo ilikuwa haijabahatika kuwa na Kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma, hivyo fursa hii ni muafaka na itakuwa na manufaa kwa watumishi wa umma na wakazi wa eneo la Kanda hiyo.
Akizungumzia uamuzi wa kujenga Kampasi hiyo wilayani Chato, Mkuchika alifafanua kuwa halmashauri ya wilaya ya Chato imetoa kiwanja hicho bure tofauti na maeneo mengine ya Kanda ya Ziwa ambayo yangekigharimu chuo fedha nyingi kununua kiwanja.
Aliishukuru halmashauri kwa kutoa kiwanja na kumhimiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa hati kwani chuo kiko tayari kuanza ujenzi mapema iwezekavyo.
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dk Emmanuel Shindika aliwathibitishia wakazi wa Kanda ya Ziwa kuwa fedha za kuanza ujenzi zimeshapatikana, hivyo kinachosubirikiwa ni hati.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chato, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Medard Kalemani alimtaka Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo kuwasilisha maombi ya kupatiwa umeme katika eneo hilo ili kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa kampasi hiyo.
Akizungumzia eneo ambalo chuo kitajengwa, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel alisema ujenzi wa kampasi hiyo ukikamilika itakuwa ni chachu ya maendeleo kutokana na muingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali watakaokuja kupata mafunzo na utavutia uwekezaji.
Mhe Dkt John Pombe Magufuli, usikubali, kataa Serikali yako isijenge tawi la chuo cha Utumishi wa Umma Chatochato CHATO chato CHATO
Nadhani tuna shida ktk kuamua kipi kiwe kipaumbele cha kwanza, pili, tatu, nne nkShida ndiyo inaanzia hapo vyuo kibao vina branch kila mahali sijwahi ona watu wanahoji sasa hapo kujenga branch tu unaona maneno kibao. Pale maana yake watahudumia mikoa kama minne mitano kwa hiyo ni sawa
Si hivyo tu;kila jiji liwe na tawi lake Chato.Ata UDSM wanatakiwa kuwa na Tawi chato
Kampas lishaisha tulete watoto?
😁😁😁Kampas lishaisha tulete watoto?