Geita: Dkt. Magufuli awataka watoto wa shule waliosimama kumtazama wasome kwa bidii

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Watoto wa Kibehe, Geita walisimama barabarani kumuangalia Mgombea wa Urais Kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa anapita kuelekea Bukoba kwenye mkutano wake wa Kampeni

Dkt. Magufuli aliwataka watoto hao wasome kwa bidii kwa kuwa wao ndio marais na mawaziri wajao. Pia aliwaambia kuwa wataendelea kusoma bure. Aidha alionyeshwa kufurahi kwa watoto wale kuwa pale

Katika safari hiyo amekuwa akiwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Oktoba 28, ambapo utafanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani nchini

Kabla ya hapo Magufuli alikutana na mwalimu aliyewahi kumfundisha na alimzawada Tsh. 50,000

Your browser is not able to display this video.
 
Mh Rais ukifika kagera. Uwe na majibu yafuatayo ya kuwaambia wananchi , wapi ulipeleka pesa za tetemeko ,wapi ulipeleka fedha za corona.
 
Waliokuwa wanasema CCM haikusanyi watoto kwenye kampeni zao amewaumbua.
 
eh!....bado anaendelea kugawa rushwa tu hata katikati ya kampeni?

aisee mwacheni Lissu aendelee kusema kuhusu ufisadi nchi aisee!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…