Geita: Jela miaka 30 kubaka mhudumu wa baa

Geita: Jela miaka 30 kubaka mhudumu wa baa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
MAHAKAMA ya Wilaya ya Geita imemhukumu mkazi wa Katoro, Justini Silivini (24), kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.

pingu mkononi edited_0.jpg


Alitiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo baada ya mahakama hiyo kuridhika kuwa alimbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 21 na kumsababishia maumivu.

Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Samuel Maweda, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kosa hilo paspo kuacha shaka yoyote.

Hakimu Maweda alisema Mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili liwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.

Alisema upande wa mashtaka ulipeleka mahakamani shahidi mmoja, ambaye alithibitisha kuwa alibakwa na mshtakiwa huyo.

Aidha, Hakimu Maweda alisema mshtakiwa huyo alikwenda kwenye baa iliyopo Mtaa wa Afya Katoro, ambapo mlalamikaji (jina lake limehifadhiwa) anapofanyia kazi.

Alisema baada ya mshtakiwa kufika kwenye hiyo baa alimkuta mlalamikaji akiwa anafanya kazi zake, ndipo mshtakiwa huyo alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu, huku akiwa na kisu mkononi hadi pembeni mwa baa hiyo na kumvua nguo na kuanza kumbaka.

Aidha, alisema mlalamikaji huyo alipiga kelele ndipo wasamaria wema walifika na kumkamata mshtakiwa huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Katoro na baada ya mahojiano mshtakiwa alipelekwa katika Mahakama ya Wilaya Geita.

Awali akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Clemence Kat, alidai mahakamani kuwa Oktoba 20, mwaka 2020 maeneo ya Katoro Mkoa wa Geita, mshtakiwa alimbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 21 na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

NIPASHE
 
Kesi za kuhujumu uchumi wa nchi kwa kuitia hasara ya mabilioni serikali mtu anapewa adhabu kwenda jela miaka mitatu au faini mil 5. Lakini kesi za kipuuzi kama hizi mahakimu wanazishadadia kweli!
 
MAHAKAMA ya Wilaya ya Geita imemhukumu mkazi wa Katoro, Justini Silivini (24), kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka...
Huyo aliyebakwa Utamu aliusikia au hapana? Ukiangalia Umri wao utagundua kuwa ni Watu wazima ( Vijana ) hivyo kuniambia kuwa Mwanamke alibakwa kidogo napatwa na Ukakasi fulani vile. au alimpelekea Moto Buza kwa Mpalange na Kuharibu kabisa Miundombinu ya Kibaiolojia ya huko?
 
Si bora hata angenitafuta tu Rais wa Kununua Malaya nimtafutie Mmoja awe anambandua tena bila Malipo na Mimi ningekuwa namalizana nae kuliko huku Kubaka na sasa anaenda Kuozea Jela? Nimesikitika....!!!
Huyu Baharia mwenzenu amewaangusha sana! Aliona kutumia nguvu ni bora zaidi kuliko mpunga! Mhudumu wa bar ni tofauti kabisa na mwanafunzi. Alitakiwa amalizane nae kwa makubaliano maalum.

Ona sasa anaenda kunyea debe kwa kesi ya kipuuzi kabisa!
 
Back
Top Bottom