Geita: Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lalamikia wananchi wanaotumia muda mwingi kupiga simu ya bure

Geita: Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lalamikia wananchi wanaotumia muda mwingi kupiga simu ya bure

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
#HABARI: Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, limewalalamikia wananchi wa Mkoa huo wanaotumia muda mwingi kupiga simu ya bure ya Jeshi hilo kwa lengo la kuwasalimia Askari waliopo zamu pamoja na kuulizia uwepo wa maji ya kutosha na utayari wao, ambapo limebainisha kuwa hali hiyo inazuia wananchi wengine wenye matukio ya moto kushindwa kupata msaada.
.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Jeshi hilo, Mkoani humo, Mrakibu Hamis Dawa, ambapo amewataka wananchi wanaotaka kuwasalimia Askari wa Jeshi hilo kufika kwenye ofisi hizo, badala ya kupiga simu.

#ITVUpdates

FB_IMG_1683818112850.jpg
 
Napendekeza Geita iwe Kanda Maalum ya Kipolisi [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wasukuma bwana! 😂😂😂

Wakijichanganya tu Kwenda kusalimia uso Kwa uso,akili zitawajaa sawa!😂
 
Wanawakumbusha wajibu 😂
Geita: Aloo afande Maji
Zimamoto: unatokea wapi na nikusaidie nini?
Geita: Im from near you nauliza maji yapo ya kutosha?
Zimamoto: Ahsante kwa kujali kila kitu kipo sawa
Geita: Watoto wamekula nyumbani?
Zimamoto: Ndio
Geita: Nyongeza ya mishahara umepata?
Zimamoto: Ndio
Geita: MMwage oil na mjaze wese hakikisheni na matairi sio kipara huku njia mbovu
Zimamoto: maoni yamechukuliwa na kila kitu kipo sawa
Geita: Msalimie Shemeji

Tiiitiiiitiii
 
Yaani hawa jamaa inaonekama wanataka kuuwasha moto uwanja wa ndege pale chattle[emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Geita wana Bangeeh ya kipekee kabisa
 
Wanawakumbusha wajibu [emoji23]
Geita: Aloo afande Maji
Zimamoto: unatokea wapi na nikusaidie nini?
Geita: Im from near you nauliza maji yapo ya kutosha?
Zimamoto: Ahsante kwa kujali kila kitu kipo sawa
Geita: Watoto wamekula nyumbani?
Zimamoto: Ndio
Geita: Nyongeza ya mishahara umepata?
Zimamoto: Ndio
Geita: MMwage oil na mjaze wese hakikisheni na matairi sio kipara huku njia mbovu
Zimamoto: maoni yamechukuliwa na kila kitu kipo sawa
Geita: Msalimie Shemeji

Tiiitiiiitiii
[emoji23]
 
Back
Top Bottom