Geita: Jiko la mkaa laua Mama, watoto wawili

Geita: Jiko la mkaa laua Mama, watoto wawili

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkazi wa kijiji cha Busanda kata ya Busanda wilayani Geita Unice Kulwa(25) na wanawe wawili wamepoteza maisha baada ya kukosa hewa kutokana na kuingiza jiko la mkaa alilokuwa akipikia maharage kwenye nyumba waliyolala.

Mbali na vifo hivyo pia baba wa familia hiyo Kulwa Kamili amenusurika kifo na amelazwa kwenye kituo cha afya Katoro akiendelea kupatiwa matibabu.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 3,2021 katika kitongoji cha Shilungule kijiji cha Busanda wilayani humo.

Aliwataja watoto waliopoteza maisha kuwa ni Kamuli Kulwa(5) na Jenipha Kulwa (3)

Akielezea tukio hilo Ofisa mtendaji wa Kata ya Busanda Victoria Mapunda amesema mama huyo baada ya kumaliza kupika chakula cha usiku aliinjika maharage jikoni na kwenda kulala na saa tisa usiku mmoja wa majirani alihisi hali ya tofauti na na alipotoka nje alikutana na hali ya tofauti.

Amesema jirani huyo aliwaamsha majirani zake bila mafanikio na kuamua kugonga kwa jirani mwingine ambaye waliamua kuvunja mlango na kuingia ndani na kuwakuta wazazi hao na watoto hawajitambui huku nyumba ikiwa na joto kali.

“Majirani waliwakimbiza Zahanati ya Shilungule na walipofika mama na wanawe wawili walifariki huku baba alipewa huduma ya kwanza na kupelekwa kituo cha afya Kaqtoro na hali yake inaendelea vizuri”amesema Victoria.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuacha tabia ya kuingiza jiko ndani huku wao wakiwa wamelala na kuchukua tahadhari za majanga mengine hasa wakati huu wa msimu wa mvua ikiwa ni kuhakikisha vyoo wanavyotumia ni imara.

“Tunaelekea msimu wa mvua ,tuchukue tahadhari,vyoo viwe salama ,funikeni visima vya asili,mashimo ya mchanga na mito tuvuke kwa tahadhari”amesema Shimo

Chanzo: Mwananchi
 
Pole nyingi kwa familia, mwaka huu vifo vya aina hii vimekuwa vingi.
 
“Tunaelekea msimu wa mvua ,tuchukue tahadhari,vyoo viwe salama ,funikeni visima vya asili,mashimo ya mchanga na mito tuvuke kwa tahadhari”amesema Shimo
Huyu Shimo anasema tufukie mashimo tena.
 
Back
Top Bottom