Geita: Kaka amuua mdogo wake baada ya kufanya vibaya kwenye mtihani wa majaribio

Geita: Kaka amuua mdogo wake baada ya kufanya vibaya kwenye mtihani wa majaribio

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Shibutwa wilayani Mbogwe mkoani Geita, Ziada Masumbuko (15) ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kaka yake kwa kile kinachodaiwa ni baada ya kufanya vibaya katika mtihani wa majaribio.

Kamanda wa polisi mkoani Geita, Hendry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio lililotokea mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Shibutwe kata ya Bunigonzi wilayani Mbogwe mkoani hapa.

Akielezea tukio hilo, kamanda Mwaibambe alisema kaka wa mwanafunzi huyo aliyefahamikakwa jina la Viaga Masumbuko (29) alimpiga mdogo wake kama kumwadhibu baada ya kufanya vibaya mtihani, hali iliyosababisha mtoto huyo kufikwa na mauti.

Kwa mujibu wa kamanda, mtuhumiwa anadaiwa kumpiga mdogo wake mara kwa mara anapofanya vibaya darasani, kitendo ambacho walimu wa mwanafunzi huyo wamekuwa wakimsihi kuacha tabia hiyo bila mafanikio.

Kamanda alidai mwili wa mwanafunzi huyo umekutwa na majeruhi maeneo ya mikononi, mabegani na miguuni na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji.

Katika tukio jingine, mwanafunzi Method Hassan (12) wa darasa la saba katika shule ya msingi Kalangalala iliyopo mjini Geita ameuawa kwa kupigwa mateke na ngumi akituhumiwa kuiba Sh15,000 kwenye duka lililopo jirani na nyumba yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo lilitokea April 7 wakati mtoto huyo akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Geita.

Akielezea tukio hilo, bibi wa mtoto huyo, Grace Mathias alisema siku hiyo akiwa nyumbani saa moja asubuhi aligongewa mlang na watoto wake wanaolala chumba cha nje na alipotoka alimkuta mjukuu wake akiwa na majeraha na alipowahoji walidai amepigwa na muuza duka aliyeko jirani na nyumba yao.

“Wanadai alikuja kuwagongea asubuhi akamuita Method na kwa kuwa ana tabia ya kumtuma alitoka ndio akamtuhumu amemuibia hela. Alimfungia stoo na kumpiga na hata nilipomwambia tumpeleke hospitali hakunijibu kitu hadi mtoto wangu mwingine alipokuja wakataka kupigana ndio akatoroka,”alisema Grace.

Alisema alimpeleka mjukuu wake polisi na badaye hospitali na kufikwa na mauti wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Geita.

Chanzo: Mwananchi
 
Mmmh sad news. May their soul Rest in Peace
 
Dah..nawaza..hapo Kama Taifa tumeshapoteza nguvu Kazi mbili kwa manufaa ya kizazi kijacho..

Hapo Kama Taifa, tumepoteza wababa bora kwa familia zao kwa Miaka kadhaa ijayo..

Hapo.kama Taifa tumepoteza Rais,Waziri, Mbungee ,mjasiriamali na mfanyakzi wa kizazi kijacho..

Hapo Kama Taifa tumepoteza Daktari Bingwa, mfanyabiashara mashuhuri na mkubwa katika kizazi kijacho..

Hapo Kama Taifa tumepunguzwa idadi ya kizazi hiki na kijacho..

Ohhh..hasira plus ujinga..why sie wanyonge tu!?

Guys..katu usikubali kuwa hakimu wa maisha ya mtu..any God ndiye anayejua undani wa...

Yamkini huyo aliyefeli mtihani Kuna changamoto alikuwa anakabiliwa nazo...zikamfanya ashindwe mara kwa mara ..ama alitakiwa kupewa muda zaidi wa kujipanga n.k

Yamkini huyo alyeiba hio 15,000 aliona namna ambavyo bibi yake anateseka na maisha akaona pengine ajaribu kumsaidia..ama pengine Kuna hitaji lake la.msingi aliona familia yake haiwezi kumtekelezea akaona pengine hio ndio njia sahihi.

Lakini ni kweli kwamba huyo kaka aliyempiga mdogo wake yeye hamjawahi kufeli..huwa afeli kwenye Mambo yake ya kimsingi ya kimaisha..nani huwa anamwazibu..!?

Ni kweli kwamba Huyo mfanyabiashara hamjawahi kuiba ama kudhulumu wa ateja wake!?

Why tunajifanya watakatifu dhidi ya makosa ya wengine !?

Nahisi kuelemewa na uzuni kwa hao vijana wadogo kuzulumiwa haki zao za kuishi kwa namna hio...dah.
 
Back
Top Bottom