Geita kuwa kitovu cha uchumi Afrika Mashariki

Geita kuwa kitovu cha uchumi Afrika Mashariki

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949

Geita. Serikali imelenga kuufanya mkoa wa Geita kuwa kitovu cha uchumi ndani ya Taifa na ukanda wa Afrika Mashariki na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo hasa kwenye uwekezaji wa mwambao wa Ziwa Victoria ili kufanya mkoa huo kuwa lango la biashara.

Akizungumza na wananchi wa mkoa huo kwenye viwanja vya Kalangalala mjini Geita leo Jumamosi Oktoba 15, 2022, Rais Samia Hassan Suluhu amesema licha ya mkoa huo kuwa na fursa ya madini lakini Serikali inaona mkoa huo umekaa vizuri kwenye eneo la kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Tumieni fursa hii kwenye mwambao wa Ziwa Victoria ambalo ndilo ziwa kubwa kuliko yote Afrika, Geita sasa inaenda kuunganishwa na nchi nyingine tumeanza kujenga daraja kubwa la Kigongo Busisi hii itawaunganisha na nchi jirani na niwahakikishie kuwa daraja hili litakamilika mapema ili kuongeza chachu kwenye shughuli za kiuchumi katika mkoa huu”amesema Rais Samia

Mkuu huyo wa nchi amesema muunganiko wa mkoa wa Geta na mikoa mingine ya kanda ya Ziwa na nchi za Afrika Mashariki kupitia mtandao wa barabara na Ziwa Victoria itaimarisha Geita kuwa lango la biashara.
Akizungumzia sekta ya madini Rais Samia amesema Serikali inatambua mchango wa wananchi wa mkoa wa Geita katika ujenzi wa uchumi hasa kwa kupitia uchimbaji wa dhahabu.

Ameiagiza Wizara ya Madini kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, utafiti na biashara unafanywa kwa kazingatia kanuni, sheria na miongozo inayosimamia sekta ya hiyo.

Amesema Wizara hiyo inafanya vizuri lakini inapaswa kuongeza bidii kwenye usimamizi na kutaka elimu ya sheria na kanuni za madini itolewe kwa wachimbaji huku akitaka Wizara hiyo kushirikiana na vyombo vya dola kudhibiti vitendo vya utoroshaji madini.

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema mkoa wa Geita ni mkoa wa kwanza kwenye uzalishaji wa dhahabu hapa nchini na kusema asilimia 40 ya dhahabu inayozalishwa inatoka mkoani Geita.

Amesema wakati Rais Samia anaingia madarakani wizara hiyo ilikuwa ikikusanya Sh475 bilioni na sasa wanakusanya Sh 622bilioni kwa mwaka na mwaka huu wa fedha wamelenga kukusanya Sh800 bilioni.

Chanzo: Mwananchi
 
lisu analialia huko alipo kwa amsterdam hataki kusikia maendekeo yoyote chato
 
Haya ni manebo yanayotamkwa na wanasiasa kila wanapoenda. Utasikia mkoa huu una fursa hii na ile, serikali itafanya hiki na kile ili eneo hili kiwe kitovu cha uchumi.

Wananchi wa Geita endeleeni kupambana, msisikilize hadithi za wanasiasa, nendeni kwenye uhalisi. Tuliwahi kuambiwa:

1) Segera litakuwa soko kuu la mazao katika Afrika Mashariki. Mpaka leo imeshindikana hata kuwa soko la wilaya.

2) Kibaigwa kutajengwa soko kuu la mahindi la Afrika Mashariki. Hivi limekuwa?]

3) Mwanza litakuwa jiji la kitovu cha uchumi Afrika Mashariki. Hivi imekuwa?

4) Kigoma itakuwa Dubai ya Afrika. Hivi imekuwa?

Ebu jiulize, hivi unajua ni kwa namna gani utaifanya Geita iwe kitovu cha uchumi cha Sudan Kusini, DRC, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda? Kuwa kitovu cha uchumi hakutegemea kauli za wanasiasa bali hutegemea uwingi na ubora wa shughuli za biashara.
 
Hakika Biteko unamsaidia vizuri sana Mhe.Rais wa JMT Mama Yetu Mpendwa Mhe.Samia Suluhu Hasan katika sekta hii ya Madini kutoka kuchangia 4% hadi 8% ya pato la Taifa hakika si kazi nyepesi lakini umeweza na pasina shaka 2025 hiyo 10% itafikiwa Mungu awape afya njema .Inshallah Geita itaenda kuwa kitovu cha Uchumi ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu.
 
Kwa kadri ambavyo Geita itapaa kuwa kitovu kikuu cha uchumi kanda ya ziwa ndivyo Mwanza itapwaya, kama ilivyo Dar kadri inavyokuwa zaidi kitovu kikuu cha Uchumi ukanda wa pwani ndivyo Zanzibar (Unguja), mkoa wa Pwani na Morogoro inapwaya, ama kwa Kadri Arusha inavyokuwa kitovu kikuu cha Utalii kwa kanda ya kaskazini ndivyo ambavyo Manyara na Kilimanjaro itapwaya. Kwanini? Huwezi kuwa na vitovu viwili vya kiuchumi katika eneo moja la kijiografia lenye mfanano au mkaribiano.

Mantiki ya eneo kuwa kitovu ni kuwa katikati, kiunganishi au kirejeo (reference point). Unaweza kuyafanya maeneo mengi kuwa vitovu lakini kwa shughuli (sekta) mahsusi tu.
 
Tatizo kubwa la serikali ya Tanzania ni kukosa focus&consistency ya vitu inavyovifanya.

Kwa mfano, kama lengo la serikali lilikuwa ni kuufanya mkoa wa Geita kuwa kitovu kikuu cha kiuchumi katika mwambao wa ziwa victoria, basi haya yangepaswa kufanyika hapo kabla.

1. Ule uwanja mkubwa wa ndege uliojengwa Chato ulipaswa kujengwa Geita mjini.

2. Mipango ya kujenga uwanja mkubwa wa kisasa wa mpira kule Chato ingehamishiwa kuwa Geita mjini.

3. Miundo mbinu mbalimbali ya majenzi (ikiwemo miradi ya NHC, TRA) ingejikita zaidi Geita mjini badala ya Chato.

4. Ile hospitali kubwa ya kisasa iliyojengwa Chato ilipaswa kujengwa Geita mjini.
 
Kigoma waliambiwa hivyo kipindi cha "Shemeji" na kipindi cha "Mjomba", wa sasa hivi wafanye kwa vitendo sasa tofauti na hapo ni chai isiyokua na sukari
Wasukuma wao walikua wanaambiwa Pamba Ni White Gold 😁😁😁, hawataki hata kusikia hizo story.
 
Haya ni manebo yanayotamkwa na wanasiasa kila wanapoenda. Utasikia mkoa huu una fursa hii na ile, serikali itafanya hiki na kile ili eneo hili kiwe kitovu cha uchumi.

Wananchi wa Geita endeleeni kupambana, msisikilize hadithi za wanasiasa, nendeni kwenye uhalisi. Tuliwahi kuambiwa:

1) Segera litakuwa soko kuu la mazao katika Afrika Mashariki. Mpaka leo imeshindikana hata kuwa soko la wilaya.

2) Kibaigwa kutajengwa soko kuu la mahindi la Afrika Mashariki. Hivi limekuwa?]

3) Mwanza litakuwa jiji la kitovu cha uchumi Afrika Mashariki. Hivi imekuwa?

4) Kigoma itakuwa Dubai ya Afrika. Hivi imekuwa?

Ebu jiulize, hivi unajua ni kwa namna gani utaifanya Geita iwe kitovu cha uchumi cha Sudan Kusini, DRC, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda? Kuwa kitovu cha uchumi hakutegemea kauli za wanasiasa bali hutegemea uwingi na ubora wa shughuli za biashara.
Bila kuisahau kagera, mkoa wenye kupakana na nchi nyingi za Africa Mashariki
 
Back
Top Bottom