TANZIA Geita: Madiwani wawili wateule wa CCM wafariki dunia

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Haya sasa, uchaguzi mdogo kabla hata ya uapisho.
---
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita kimepata pigo baada ya madiwani wake wawili wateule kufariki dunia kwa nyakati tofauti wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi Novemba 7, 2020 katibu mwenezi wa CCM mkoani Geita, David Azaria amewataja madiwani hao wateule kuwa ni Masalu Luponya (Bugalama) na Magomamoto Zanziba (Buziku).

Azaria amesema Luponya aliugua wakati wa kampeni na hata siku ya uchaguzi Oktoba 28, 2020 alipigiwa kura na wananchi akiwa amelazwa hospitali ya Bugando.

Amesema Magomamoto aliugua ghafla juzi na alipelekwa Bugando lakini alifariki saa chache baadaye.

Amesema Luponya atazikwa leo nyumbani kwake Bugalama huku taratibu za mazishi ya Magomamoto zikiendelelea kufanywa na chama hicho kwa kushirikiana na familia yake.

Magomamoto alikuwa diwani wa Buziku kuanzia 2010 hadi 2020 na mwaka 2010 hadi 2015 alikuwa makamu mwenyekiti wa baraza la madiwani.

Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Geita, Jonathan Masele amesema kifo cha Luponya ni pigo kwa CCM na jamii iliyokuwa ikimzunguka.

Luponya wakati wa uhai wake alikua akisomesha wanafunzi 50 wa sekondari na 20 wa ualimu sambamba na kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwenye kata hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Nili-comment katika uzi mmoja hapa nikisema hata wale wa Mjengoni wanaweza kuwa wanapukutika tu kila siku.

Huo uchaguzi mdogo wawachachie tu CCM waendelee kufurahia.
Mbona ushabiki wa kisiasa unawatoa utu kiasi hiki aisee
 
Kama hawakukumbuka kutubu dhambi zao za wizi wa kura walizoiba hawawezi kupumzika kwa amani.

Hakuna ajuae kama kweli waliiba, hakuna anayejua kama walikufa na dhambi, na hakuna sababu ya kuwahukumu marehemu kwa kuwatakia mabaya

Tujiulize sisi tuko sawa na Mungu kwa kila neno? Na tutaondokaje?
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita kimepata pigo baada ya madiwani wake wawili wateule kufariki dunia kwa nyakati tofauti wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Geita. Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita kimepata pigo baada ya madiwani wake wawili wateule kufariki dunia kwa nyakati tofauti wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi Novemba 7, 2020 katibu mwenezi wa CCM mkoani Geita, David Azaria amewataja madiwani hao wateule kuwa ni Masalu Luponya (Bugalama) na Magomamoto Zanziba (Buziku).

Azaria amesema Luponya aliugua wakati wa kampeni na hata siku ya uchaguzi Oktoba 28, 2020 alipigiwa kura na wananchi akiwa amelazwa hospitali ya Bugando.

Amesema Magomamoto aliugua ghafla juzi na alipelekwa Bugando lakini alifariki saa chache baadaye.

Amesema Luponya atazikwa leo nyumbani kwake Bugalama huku taratibu za mazishi ya Magomamoto zikiendelelea kufanywa na chama hicho kwa kushirikiana na familia yake.

Magomamoto alikuwa diwani wa Buziku kuanzia 2010 hadi 2020 na mwaka 2010 hadi 2015 alikuwa makamu mwenyekiti wa baraza la madiwani.

Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Geita, Jonathan Masele amesema kifo cha Luponya ni pigo kwa CCM na jamii iliyokuwa ikimzunguka.

Luponya wakati wa uhai wake alikua akisomesha wanafunzi 50 wa sekondari na 20 wa ualimu sambamba na kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwenye kata hiyo.
 
Mbona wizi uko wazi? Jamaa zangu niliokuwa nao serikalini wanakiri kabisa kwamba wameshirikishwa dhambi ya kipumbavu kabisa! Hawa wafe tu hamna namna tutawahurumia! Hata akidondoka yule mwenyekiti wao kwetu itakuwa burudani tu!
Polisi ndo wamefanikisha ushindi wa ccm so ccm isiwasaahau police kuwaboreshea maslai yao,
Isiwatumie tu nyakati za uchagu then ikawadump
 
Back
Top Bottom