Unajianika ujinga na ukatili ulionao ?Huwa nawashauri watoe ushirikiano kwenye vyombo sahihi ili hayo matukio yafanyiwe kazi.
Wasiwafiche mashahidi wala suluhu sio wakimbilie ubelgiji na kwenda kutoa taarifa BBC, Al Jazeera, DW.... na kwingineko ambako hadi sasa hawajawasaidia chochote
Mjinga ni wewe unayeamini vitu visivyoelewekaUnajianika ujinga na ukatili ulionao ?
Kwa kidhungu inaitwa double D....dabulo deefi.... huwezi kukata rufaa kwa kifo ..tuna tume_ccm,police_ccm n.k contrary hakuna mungu_ccm wasipumzike kwa amani.Haya sasa, uchaguzi mdogo kabla hata ya uapisho.
---
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita kimepata pigo baada ya madiwani wake wawili wateule kufariki dunia kwa nyakati tofauti wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi Novemba 7, 2020 katibu mwenezi wa CCM mkoani Geita, David Azaria amewataja madiwani hao wateule kuwa ni Masalu Luponya (Bugalama) na Magomamoto Zanziba (Buziku).
Azaria amesema Luponya aliugua wakati wa kampeni na hata siku ya uchaguzi Oktoba 28, 2020 alipigiwa kura na wananchi akiwa amelazwa hospitali ya Bugando.
Amesema Magomamoto aliugua ghafla juzi na alipelekwa Bugando lakini alifariki saa chache baadaye.
Amesema Luponya atazikwa leo nyumbani kwake Bugalama huku taratibu za mazishi ya Magomamoto zikiendelelea kufanywa na chama hicho kwa kushirikiana na familia yake.
Magomamoto alikuwa diwani wa Buziku kuanzia 2010 hadi 2020 na mwaka 2010 hadi 2015 alikuwa makamu mwenyekiti wa baraza la madiwani.
Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Geita, Jonathan Masele amesema kifo cha Luponya ni pigo kwa CCM na jamii iliyokuwa ikimzunguka.
Luponya wakati wa uhai wake alikua akisomesha wanafunzi 50 wa sekondari na 20 wa ualimu sambamba na kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwenye kata hiyo.
Chanzo: Mwananchi
Mods wamefuta comments zote za namna hii!Huu uzi ungekuwa uko page ya 12 sasa!Hata hii comment yako baadae wataifuta!Uzuri ni ccm acha wafe tu
Siku jiwe akifa nisisherehekee?Kwakweli ninaweza kujizuia kwa muda kama mtu aliyebanwa na cheko halafu akaibana,kadri sekunde zinavyoenda ndio unaanza kuona sura yenyewe inamkatili na hatimaye inaanguka cheko lenyewe!Hakuna ajuae siku wala saa Mwenyezi Mungu aziweke mahala pema roho zao
Katika kitu ambacho sikiwezi kabisa ni kufurahia kifo cha binadamu mwenzangu
Tena wazikwe na zege wasije wakaamkaMods wamefuta comments zote za namna hii!Huu uzi ungekuwa uko page ya 12 sasa!Hata hii comment yako baadae wataifuta!
Hiyo ndio hali halisi ndio matunda ya chukiKwani Tundu amekufa nikafurahia???
Huoni kama hao wanaomtishia ni sawa wawekwe hadharani ili washughulikiwe?
Acha kujichanganya utachanganyikiwa bure