Geita: Mchungaji ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumnyonga

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mchungaji wa Kanisa la Habari Njema, Kasese Gervas Bilalo (47), kwa tuhuma za kumuua mke wake, Martha Faustine (45).

Inadaiwa mtuhumiwa alimvizia mkewe akiwa amelala, akamkaba kwa kutumia kamba ya katani kabla ya kumning’iniza juu ya kenchi ya nyumba waliyokuwa wakiishi ) katika Kijiji cha Nyarututu, wilayani Chato.

Kwa mujibu wa taarifa za awali za Jeshi la Polisi, uchunguzi umeonesha kuwa mazingira ya tukio hilo yalitengenezwa ili yaonekane kama kujinyonga.

Chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa ni migogoro ya kifamilia iliyotokana na tuhuma za mahusiano ya nje ya ndoa dhidi ya mchungaji huyo.

Tukio hilo lilibainika Mei 12, 2026 majira ya saa 6:00 mchana baada ya marehemu kukutwa amefariki ndani ya nyumba yao.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa uchunguzi zaidi huku mtuhumiwa akiendelea kuhojiwa na Polisi.
 
Walokole walipaswa wawe mirembe ni vile basi tu hatupo makini na afya ya akili
20260512_120551.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mchungaji wa Kanisa la Habari Njema, Kasese Gervas Bilalo (47), kwa tuhuma za kumuua mke wake, Martha Faustine (45).

Inadaiwa mtuhumiwa alimvizia mkewe akiwa amelala, akamkaba kwa kutumia kamba ya katani kabla ya kumning’iniza juu ya kenchi ya nyumba waliyokuwa wakiishi ) katika Kijiji cha Nyarututu, wilayani Chato.

Kwa mujibu wa taarifa za awali za Jeshi la Polisi, uchunguzi umeonesha kuwa mazingira ya tukio hilo yalitengenezwa ili yaonekane kama kujinyonga.

Chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa ni migogoro ya kifamilia iliyotokana na tuhuma za mahusiano ya nje ya ndoa dhidi ya mchungaji huyo.

Tukio hilo lilibainika Mei 12, 2026 majira ya saa 6:00 mchana baada ya marehemu kukutwa amefariki ndani ya nyumba yao.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chato kwa uchunguzi zaidi huku mtuhumiwa akiendelea kuhojiwa na Polisi.
Kawaida mtu anayejinyonga mwenyewe akiwa hai lazima haja zimtoke
 
Back
Top Bottom